Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 12:47

Upinzani wadai EAC imeshindwa kusuluhisha mgogoro wa Burundi


Wakimbizi wa Burundi
Wakimbizi wa Burundi

Kikao cha 5 cha mazungumzo ya kumaliza mgogoro wa Burundi kimemalizika Jumatatu mjini Arusha ambapo upande wa upinzani wamedai kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imeshindwa kusuluhisha mgogoro wa Burundi.

Msuluhishi wa kikao hicho Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa, ameeleza kwamba amekamilisha kazi aliyo kuwa amepewa.

Amesema atakabidhi mapendekezo yaliotolewa wakati wa kikao hicho na wapinzani na mapendekezo ya serikali ya Burundi yaliyo tolewa kwa maandiko kwa Rais Yoweri Museveni ambaye ni msuluhishi mkuu, ili aamuwe kitakachofuatia.

Lakini ofisi ya usuluhishi imesema kuwa wawakilishi wa serikali ya Burundi hawakushiriki katika mazungumzo hayo.

Chauvineau Mugwengezo ambaye ni mwenyekiti wa chama cha upinzani UPD, amesema tamko la Rais Mkapa linadhihrisha kuwa viongozi wa Afrika Mashariki hawakuwajibika katika kazi yao.

Mungwegezo ameongeza kuwa wapinzani wa ndani na nje ya Burundi wameomba mchakato wa kusuluhisha mgogoro wa Burundi uondolewe kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki na ukabidhiwe Umoja wa Afrika.

Pamoja na mapungufu hayo, wapinzani wanaeleza kuwa mapendekezo walio yawasilisha kwa msuluhishi yanaweza kuchangia katika kutatua mgogoro wa kisiasa unaoisibu Burundi.

Baadhi ya mapendekezo hayo, ni kutengeneza mazingira ya usalama ili wanasiasa walio uhamishoni na wakimbizi waweze kurejea nchini, kuwaachia huru wafungwa wote wa kisiasa, na kuunda serikali inayojumuisha pande zote katika hali ya kuanda uchaguzi ulio huru na wahaki.

Mzozo wa Burundi ulilipuka mwezi April mwaka 2015 baada ya Rais Pierre Nkurunziza ambaye anaiongoza Burundi tangu mwaka 2005, kuchukuwa hatua ya kuwania muhula wa tatu, hatua iliotajwa na wapinzani wake kwamba inakiuka katiba ya nchi.

Lakini wafuasi wa Nkurunziza wanasema Mahakama ya Katiba ya nchi hiyo iliamuru kwamba Rais anaruhusiwa kuwania muhula mwengine.

Mgogoro huo ulisababisha vifo vya ma miya ya watu, na wengine takribani laki nne kuhama makazi yao na kukimbilia katika nchi jirani, wengi wao wakiwa bado nchini Tanzania.

XS
SM
MD
LG