Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 02:11

Mshukiwa wa mauaji ya kimbali akamatwa Afrika ya Kusini


Wanavijiji wakichimba kutafuta mabaki ya wahanga wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, tarehe 5, 2023. Picha na Clement DI ROMA / AFP.
Wanavijiji wakichimba kutafuta mabaki ya wahanga wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, tarehe 5, 2023. Picha na Clement DI ROMA / AFP.

Mnyarwanda anayetuhumiwa kuamuru mauaji ya Watutsi wapatao 2,000 waliokimbilia kanisani kutafuta hifadhi wakati wa mauaji ya kimbari ya 1994 amekamatwa nchini Afrika Kusini, mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Uhalifu wa Kivita uliotendwa nchini Rwanda ilisema siku ya Alhamisi.

Afisa wa zamani wa polisi Fulgence Kayishema amekuwa mafichoni tangu mwaka 2001, wakati Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji kwa Rwanda (ICTR) ilipomfungulia mashtaka ya mauaji ya kimbari kutokana na jukumu lake kwa uharibifu uliofanyika katika Kanisa Katoliki la Nyange lililoko katika Jimbo la Kibuye.

"Kukamatwa kwake hatimaye kunahakikisha kuwa haki itatendeka kuhusiana na shutuma kwa uhalifu wake," mwendesha mashtaka Serge Brammertz katika mahakama ya kimataifa ya utaratibu wa mabaki kwa mahakama za uhalifu (IRMCT), ambao umechukua nafasi ya ICTR tangu ilipofungwa mwaka 2008.

Kayishema anatarajiwa kuhamishiwa Rwanda kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka wakati Umoja wa Mataifa umesema mwaka 2012 kesi yake ilipelekwa kwa mamlaka ya Rwanda.

Akitoa maoni yake mara baada ya kukamatwa kwa Kayishema, msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo aliandika katika mtandao wa Twitter: "Hatimaye."

Inakadiriwa kuwa watutsi 800,000 na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, yaliyoratibiwa na utawala wa kihutu uliokuwa na msimamo mkali, na kutekelezwa na maafisa wa kieneo na raia wa kawaida katika jamii yenye matabaka ya juu.

Fulgence Kayishema (juu kulia) kwenye bango la arodha ya wanaotafutwa. Picha na Mariam KONE / AFP.
Fulgence Kayishema (juu kulia) kwenye bango la arodha ya wanaotafutwa. Picha na Mariam KONE / AFP.

Kayishema alikuwa katika orodha ya watu wanaotafutwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani chini ya Mpango wa Tuzo kwa Haki, na tuzo ya dola millioni tano kutolewa kwa atakayesaidia kukamatwa kwake.

Brammertz alisema uchunguzi uliopelekea kukamatwa kwake ulisambaa katika nchi kadhaa barani Afrika na kwingineko, na iliwezekana kupitia msaada na ushirikiano wa mamlaka za Afrika Kusini.

Mwezi Mei mwaka 2020, mhusika mwingine mkuu aliyepanga mauaji ya kimbari, Felicien Kabuga, alikamatwa nchini Ufaransa baada ya kuwa mafichoni kwa miaka 26.

Kukamatwa kwa Kayishema sasa kunamaanisha kuna watuhumiwa watatu waliobaki mafichoni wanaoshitakiwa na mahakama ya kimataifa ambao bado hawajulikani walipo, ingawa msemaji wa serikali ya Rwanda amesema wanafikiria kuwa idadi kubwa ya washukiwa bado wako mafichoni.

Forum

XS
SM
MD
LG