Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 21:27

Mradi wa Total wa bomba la mafuta Tanzania: 'unamadhara yasiyokubalika kwa mazingira na binadamu '


Makao Makuu ya kampuni ya TotalEnergies
Makao Makuu ya kampuni ya TotalEnergies

Mradi mkubwa na wenye utata wa mafuta wa Afrika Mashariki unaoongozwa na kampuni kubwa ya mafuta ya Ufaransa TotalEnergies unaweza kuhatarisha uharibifu “usiokubalika”, ripoti ya jumuiya mbili  sisizo za kiserikali zimeonya Jumatano.

Total na Kampuni ya Kitaifa ya China ya Mafuta (CNOOC) zimesaini mkataba wa dola bilioni 10 mapema mwaka huu kuendeleza vitalu vya mafuta Uganda na kusafirisha mafuta ghafi kupitia bomba lenye urefu wa kilomita 1,445 (Maili 900) hadi Bandari ya Tanga iliyoko katika Bahari ya Hindi.

Mradi huo mkubwa umekabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa wanaharakati na vikundi vya mazingira, wakisema unahatarisha maisha ya maelfu ya watu na kuharibu mifumo dhaifu ya mazingira katika kanda.

Ripoti hiyo ya asasi ya kiraia ya Friends of the Earth and Survie(Survival) ilisema bomba hilo litatoa hadi tani milioni 34 za hewa chafu ya kaboni kila mwaka kuchafua mazingira – kwa wingi zaidi kuliko ukichanganya gesi chafu zinazozalishwa viwandani nchini Uganda na Tanzania.

Imetahadharisha miundo mbinu ya usafirishaji wa mafuta ghafi Afrika Mashariki ina hatari ya kuleta ajali kubwa ya kuvuja mafuta katika pwani ya Tanzania na huenda ikaleta madhara kwa maeneo yanayohifadhiwa ya baharini, na kutishia usalama wa zaidi ya kilomita za mraba 2,000 za hifadhi za asili” katika nchi yenye viumbe hai mbalimbali.

Ripoti hiyo ilisema jamii zimelazimika kutoa ardhi zao “kwa kulazimishwa na kwa bei isiyo ya haki… kuipa ushirika wa EACOP unaoongozwa na Total.”

Watu hao wanakabiliwa “na ucheleweshaji wa muda mrefu” kupata fidia zao, imeongeza ---” miaka mitatu hadi minne kwa wengi wa wale walioathiriwa”.

Asasi za kiraia zilisema TotalEnergies walikuwa “ hawajatekeleza hatua za kutosha kusitisha ukiukaji huu”, na kuhitimisha kuwa “ itagharimu maisha ya binadamu, hali ya hewa na mazingira kwa kutekelezwa mradi mkubwa huu wa Total kitu hakikubaliki”.

Wakijibu tuhuma hizi, Total Energies walisema “watafanya kila kinachowezekana mradi huu uwe ni mfano kwa kuuweka wazi, kugawana maslahi, uchumi na maendeleo ya jamii, maendeleo endelevu, uhamasishaji wa utunzaji wa mazingira na kuheshimu haki za binadamu.

FILE - Bunge la Ulaya likikutana Sept. 14, 2022, huko Strasbourg, eastern France.
FILE - Bunge la Ulaya likikutana Sept. 14, 2022, huko Strasbourg, eastern France.

Mwezi iliyopita, Bunge la Umoja wa Ulaya lilipitisha azimio lililokuwa limeeleza wasiwasi kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu.”

Haya ni pamoja na “ kufungwa kimakosa kwa watetezi wa haki za binadamu, kusimamishwa shughuli za asasi za kiraia kiholela, kuhukumiwa kwenda jela kiholela na kuondolewa kwa mamia ya watu kutoka katika ardhi zao bila ya fidia ya haki na ya kutosha.”

Siku ya Jumanne, polisi mjini Kampala iliwakamata wanafunzi kadhaa wa Uganda wakati wakiandamana dhidi ya mradi huo.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Kikundi cha Kampeni cha StopEACOP kimetaka wanafunzi hao “waachiwe mara moja”.

Mtatibu Omar Elmawi alisema:” Inasikitisha kuwa katika zama zetu, raia wasiokuwa na hatia wanakamatwa kwa sababu wanatumia haki zao za kupaza sauti.. juu ya mradi wa EACOP na madhara itakayosababisha kwa watu, mazingira na hali ya hewa.”

Azimio la Bunge la Ulaya lilisema zaidi ya watu 100,000 walikuwa hatarini kukoseshwa makazi yao kutokana na bomba la mafuta na kutaka watu hao wafidiwe vya kutosha.

Pia imehimiza TotalEnergies kuchukua mwaka mzima kabla ya kuzindua mradi huu kufanya uchambuzi yakinifu iwapo kuna njia mbadala “ya kulinda viumbe hai na vyanzo vya maji iliyobora zaidi katika maeneo ya Uganda na Tanzania.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG