Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 09, 2023 Local time: 02:39

Magufuli, Museveni wazindua mradi wa mafuta


Rais John Magufuli na Rais Yoweri Museveni

Marais wa Uganda Yoweri Museveni na Pombe Magufuli, wamezindua ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka wilayani Hoima magharibi mwa Uganda hadi Tanga nchini Tanzania.

Marais hao wamezindua ujenzi wa kilomita 1445 za bomba la kusafirisha mafuta kutoka Hoima, hadi bandari ya Tanga, nchini Tanzania.

Katika sherehe fupi kwenye mpaka wa Uganda na Tanzania wa Mutukula, wilayani Kyotera nchini Uganda, serikali ya Uganda imeeleza furaha kutokana na uzinduzi huo na kusisitiza manufaa yake.

Medard Kalemani waziri wa nshati wa Tanzania ameeleza manufaa ya mradi huo.

“Bomba hilo ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi zetu mbili. Ujenzi huu utahusisha mambo matatu makubwa. La kwanza ni ujenzi wa bomba lenyewe, ujenzi wa vituo vya mafuta na la tatu ni ujenzi wa mapipa ya kuchukulia mafuta kule tanga”

Rais Museveni aliamua kumwachia mgeni wake, John Mgufuli, kuzungumza aliyesisitiza kwamba Uganda ilifanya uamuzi wa busara kuchagua bomba hilo kujengwa ndani ya Tanzania.

“ukweli usiofichika ni kwamba Tanzania ni nchi salama. Wanasiasa wa Tanzania ni wapole tena wakarimu. Hawana matatizo. Kwa hivyo hata bomba likipita hapa, hakuna usumbufu.

Na nawaahidi kwamba chini ya utawala wangu na Yule atakayekuja baada yangu, bomba hili litakaa salama salmini bila tatizo kwa sababu bomba hili limekuja kwa wakati tunapolitaka sana”

Uganda ilikuwa imeamua kujenga bomba hilo kuelekea Kenya lakini mipango hiyo ikafutiliwa mbali. Kwake rais Magufuli, uamuzi wa museveni ulikuwa mgumu lakini unalinganishwa na hatua ya Uganda kuipigia Tanzania ahsante, kwa mchango wa kisiasa Tanzania ilitekeleza ndani ya Uganda.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG