Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 12:44

Mkutano wa G20 wajadili namna ya kukabiliana na janga la corona


Picha za viongozi wa G20 waliohudhuria mkutano kwa njia ya video.(Photo by Handout / Palazzo Chigi press office / AFP) /

Rais Xi Jinping wa China ametoa wito wa kuwepo ushirikiano thabiti wa kimataifa ili kupambana na janga la COVI-19 alipokutana na viongozi wa mataifa tajiri duniani, G20, katika mkutano wa dharura kupitia mawasilianio ya video, wakijadili namna ya kukabiliana na janga hilo.

Xi amependekeza mambo manne muhimu wakati wa mkutano huo ikiwa ni pamoja na mawaziri wa afya wa kundi lao la G20 kukutana kwa haraka iwezekanavyo kujadili hatua zinazohitaji kuchukuliwa, kuimarisha kubadilishana habari na na kushirikiana katika kupata tiba, chanjo na kudhibiti ugonjwa huo.

Vile vile, rais huyo alipendekeza kwa mataifa tajiri kusaidia mataifa maskini kuimarisha mifumo yao ya afya.

Zaidi ya Hayo kiongozi wa China alitaka mataifa ya kundi hilo kusaidia mashirika ya kimataifa kupambana kikamilifu na mlipuko huo, na kuahidi msaada wa China kulisaidia Shirika la Afya, WHO, kuongoza juhudi za kimataifa kupatikana tiba.

Pia Xi alitaka G20 kuongeza juhudi zake kuratibu sera za kiuchumi katika kupunguza athari zinazotokana na janga hili na kuepusha uchumi wa dunia kudumaa.

Mkutano huo ulisimamiwa na Saudi Arabia ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa G20, na uliitishwa kwa dharura na Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud ili kutafuta njia za kuzuia janga hilo na kukabiliana na athari zake za kiuchumi.

Viongozi wa G20 waliungana baadae na mataifa kadhaa yaliyo alikwa ikiwa ni pamoja na Syria Jordan, Singapore na Uswisi, pamoja na wakuu wa mashirika mengine ya kimataifa na kikanda.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG