Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 05:08

COVID-19 : Rais wa China asema yuko tayari kuisaidia Marekani


Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa China Xi Jinping.

Rais wa China amemwambia rais wa Marekani Ijumaa kuwa China iko tayari kutoa msaada kwa Marekani katika kupambana na virusi vya corona aina ya COVID-19.

China ilikuwa ndio chimbuko la mlipuko wa ugonjwa huo, na hivi sasa Marekani ndio inaongoza kwa maambukizo.

Mapema Ijumaa Marekani ilikuwa na wagonjwa 85,991 waliothibitishwa kuwa na maambukizo ya virusi hivyo, China ilikuwa na wagonjwa 81,828, na Itali, ambayo ni chimbuko la maambukizi bara la Ulaya, ilikuwa na wagonjwa 80,589, kwa mujibu wa kituo cha kufuatilia virusi vya Corona cha Johns Hopkins.

Baada ya mazungumzo ya simu na Xi, Trump aliyaweka katika akaunti yake ya Twitter: “Nimemaliza kufanya mazungumzo na Rais Xi (Jinping) wa China. Tumezungumza kwa urefu juu ya virusi vya corona ambavyo vimeleta maangamivu katika maeneo makubwa ya dunia yetu.

China imepitia mengi na imeweza kujenga uelewa mkubwa wa virusi hivi. Tunashirikiana kwa karibu. Tunawaheshimu sana!”

Katika mikutano yake na waandishi wa habari, Rais wa Marekani hakuonyesha “heshima ya kutosha” kwa China, akitoa kauli za kudhihaki juu ya nchi hiyo ya Asia ilivyokabiliana na mlipuko huo. Kiongozi huyo wa Marekani alikuwa akiita virusi hivyo ni “Virusi vilivyoanzia China.”

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG