Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 18:47

Ethiopian Airlines yajikita kusafirisha mizigo kukabiliana na athari za corona


Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ethiopia.
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ethiopia.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la ndege la Ethiopian Airlines Tewolde Gebremariam anasema shirika lake hivi sasa linajikita kusafirisha mizigo badala ya abiria ikiwa ni hatua ya kujikwamua kiuchumi kutokana na athari za maambukizi ya virusi vya corona.

Hatua hii imechukuliwa kwa lengo la kukabiliana na athari kubwa inayo yakabili mashirika ya ndege kutokana na janga la virusi vya corona lililopelekea mashirika mengi ya ndege kuahirisha safari zake.

Abiria wengi wamesitisha kusafiri ikiwa ni hatua ya kuepuka misongamano ya aina yoyote ikiwemo safari za ndege.

Akizungumza na shirika la habari la Reuters, anasema hivi sasa wanageuza malengo yao yote na rasilmali zao kwa kujikita kusafirisha mizigo ambapo anasema wanageuza ndege 10 aina ya Boeing 777 na mbili za 737 kuwa mizigo kuelekea maeneo yote ya dunia kila siku.

Janga la COVID-19 limesababisha hasara kubwa ya kifedha kwa sekta ya usafiri wa ndege na mamlaka ya usafiri wa ndege wa kimataifa IATA inasema mashirika ya ndege ya Afrika yatapoteza karibu dola bilioni 4.4 baada ya maelfu ya safari kufutwa.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG