Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 12:02

Mkutano wa EAC waahirishwa kwa kukosekana Nkurunzinza


Rais Pierre Nkurunzinza

Mkutano wa 20 wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa umepangwa kufanyika Ijumaa jijini Arusha, kaskazini mwa Tanzania, umeahirishwa baada ya Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza kushindwa kuhudhuria wala kutuma mwakilishi.

Akitoa taarifa ya kuahirishwa kwa mkutano huo Mwenyekiti wa baraza la Mawaziri wa nchi hizo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Augustino Mahiga, amesema koram ya mkutano ilikuwa haijakamilika.

Wakizungumza baada ya kuahirishwa kwa mkutano huo baadhi ya washiriki akiwemo mkurugenzi wa baraza la biashara la Afrika Mashariki Peter Mathuki amesema kuahirishwa huko hakuna athari kubwa katika sekta ya biashara.

Mkutano huo wa viongozi pamoja na masuala mengine ulikuwa ujadili mapendekezo ya kusuluhisha mzozo wa Burundi, yaliyo fikishwa na mpatanishi mkuu wa mzozo huo Rais Yoweri Museveni wa Uganda.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG