Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 27, 2023 Local time: 14:05

Tshisekedi arejea Kinshasa


Felix Tshsekedi, kulia, na Vital Kamerhe

Moja wapo ya wagombea wakuu wa upinzani katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, Felix Tshisekedi akifuatana na mgombea mwenza Vital Kamerhe wamerudi Kinshasa wakieleza matumaini ya kupata ushindi katika uchaguzi wa Disemba.

Tshisekedi alipowasili Jumanne amesema kwamba kulingana na tafiti iliyofanywa na taasisi moja ya Marekani yeye na mwenzake Kamerhe wataweza kupata karibu asili mia 50 za kura wakati wa uchaguzi wa Disemba 23.

Kiongozi huyo anasema uchaguzi ni lazima ufanyika kwa kutumia au kutotumia kompyuta zinazozusha malalamiko makubwa nchini humo kwa madai kwamba serikali inaweza kuzitumia mashine kuiba kura.

Kuna wagombea 21 wanaoshiriki katika uchaguzi huo wa rais ambapo Tshisekedi na Martin Fayulu ni wagombwa wakuu wa upinzani dhidi ya mgombea wa munagno wa vyama vya utawala Emmanuel Ramzani Shadary.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG