Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 25, 2024 Local time: 15:51

Mkataba wa hali ya hewa wafikiwa katika mkutano wa COP26


Eneo lililotengwa Action Zone likionekana wakati siku inaanza kimya katika Mkutano wa Hali ya Hewa Glasgow, Scotland, Nov. 13, 2021.
Eneo lililotengwa Action Zone likionekana wakati siku inaanza kimya katika Mkutano wa Hali ya Hewa Glasgow, Scotland, Nov. 13, 2021.

Viongozi wa dunia wamepongeza makubaliano mapya ya mabadiliko ya hali ya hewa yaliyosainiwa na karibu nchi 200 jioni Jumamosi kuharakisha hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa wakati mkutano wa COP26 ukifikia ukingoni huko Glasgow, Scotland.

Waliosaini mkataba wa Hali ya Hewa wa Glasgow wameahidi kuendelea kushirikiana kudhibiti ongezeko la joto duniani ili lisizidi nyuzi 1.5 Celsius kufikia juu ya kiwango cha kipindi kabla ya maendeleo ya viwanda, lengo lililokuwa limewekwa katika mkutano wa hali ya hewa wa Paris mwaka 2015.

Na kengele ililia ilipofika wiki mbili za mazungumzo mazito majira ya saa tatu usiku kwa saa za Scotland (9:38 p.m majira ya UTC) Jumamosi jioni, zaidi ya saa 24 baada ya mpangilio uliowekwa awali mkutano kumalizika za kumi na mbili jioni Ijumaa.

“Hii ni hatua ya kikweli kuweza kufikia kudhibiti joto kwa digree 1.5. Hatua tuliyopiga kwa pamoja. Lakini ulazima wa kuendeleza hatua na kutekeleza kuwa sambamba na matakwa lazima iendelezwe wakati wote wa muongo huu,” Rais wa COP26 Alok Sharma amewaambia wajumbe wa mkutano baada ya mkataba huo kusainiwa.

Wakati mazungumzo yakimalizika Jumamosi, hata hivyo, India na China zimesisitiza kulegeza utekelezaji wa ahadi ili kuondoa makaa ya mawe na mafuta ghafi. Ilikuwa ni sehemu ndogo lakini mabadiliko muhimu yaliyomfanya rais wa mkutano akionekana kukereka.

“Naomba radhi kwa jinsi mchakato huu ulivyotokea na naomba radhi sana,” Sharma alisema. “Pia nafahamu juu ya mfadhaiko huu wa kina. Lakini nafikiri, kama ulivyoeleza, ni muhimu pia kuwa tuulinde mkataba huu.”

India, pamoja na China na Afrika Kusini, wamelalamika kuwa kuondoa kwa mafuta ghafi kuwa sio haki. Takriban asilimia 70 ya nishati ya India inategemea makaa wa mawe.

“Vipi mtu anaweza kutegemea kuwa nchi zinazoendelea ziweke ahadi za kuondoa matumizi ya makaa ya mawe na ruzuku ya mafuta ghafi? Nchi zinazoendelea bado ni lazima washughulikie ajenda yao ya maendeleo na utokomezaji wa umaskini,” Waziri wa Mazingira wa India Bhupender Yadav amesema.

Habari hii imechangiwa na Mashirika ya Habari Reuters na AP

XS
SM
MD
LG