Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 09:52

COP26 : Kijana wa Afrika azitaka nchi tajiri kutekeleza ahadi zao


Ramani ya Ziwa Chad, na nchi zinazoizunguka ikiwemo Chad, Niger, Nigeria na Cameroon
Ramani ya Ziwa Chad, na nchi zinazoizunguka ikiwemo Chad, Niger, Nigeria na Cameroon

Afrika iko katika mstari wa mbele kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa. Hakuna mahali ushuhuda huu uko wazi zaidi kuliko katika Bonde la Ziwa Chad, ambalo limechukua takriban asilimia 8 ya bara hilo na kuwasaidia mamilioni ya watu.

Umoja wa Mataifa unasema Ziwa hilo limepungua kwa asilimia 90 tangu miaka ya 1960 kwa sababu ya ukame.

Matokeo ya ushindani wa mali ghafi umesababisha umaskini na migogoro. Zaidi ya watu milioni 10 wanategemea misaada ya kibinadamu.

Oladosu Adenike, miaka 27, ameshuhudia yeye mwenyewe maafa ya mabadiliko ya Ziwa Chad. Ni mfanya kampeni maarufu juu ya mabadiliko ya hali ya hewa Afrika na ameanzisha Kampeni ya Nigeria “Ijumaa kwa ajili ya mustakbali”, akiungana na harakati za kimataifa baada ya kukutana na mwanaharakati wa Sweden Greta Thunberg.

Adenike ni mmoja wa vijana kadhaa katika ujumbe wa Afrika aliyesafiri maelfu ya maili hadi Glasgow, Scotland, kuwa ni sehemu ya mkutano wa hali ya hewa COP26 na kufikisha hisia za dharura kwa viongozi wa dunia.

“Usalama na utulivu katika eneo hilo – huko Mkoa wa Ziwa Chad, eneo la Sahel – unategemea pale tunapoweza kuimarisha ziwa hilo na kuweza kusema kuwa watu wanaweza kupata mahitaji endelevu ya maisha, kuwa wasiwe hatarini kujiunga na vikundi vya watu wenye silaha. Na hili wakati huo huo litaboresha demokrasia katika eneo.

Adenike ni afisa kijana wa ujumbe wa Nigeria katika mkutano wa COP26 na amehutubia wajumbe wa ngazi ya juu ulazima wa kuchukua hatua za haraka. Lakini anasema anakatishwa tamaa na hatua zinazosuasua.

“Bado tuko katika awamu ya mazungumzo. Hatuingia katika awamu ya kuchukua hatua, ambayo inahitaji hivi sasa ifanyike, na kutoahirisha hadi siku za usoni. Kwa sababu hilo ni jambo hatari zaidi kulifanya hivi sasa. Kuchelewesha hivi sasa hatua hiyo ni kukanusha mgogoro wa hali ya hewa,” Adenike amesema.

Kaluki Paul Mutuku ni mjumbe kijana kutoka Kenya. Kama Adenike, ni Sauti maarufu ya kijana anayepigania udhibiti wa mabadiliko ya hali ya hewa Afrika.

XS
SM
MD
LG