Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 06, 2022 Local time: 09:44

Misri yafunga kivukio kikuu kwenye mpaka na Ukanda wa Gaza


Kivukio cha Rafah

Misri ilifunga kivuko chake kikuu cha mpaka na ukanda wa Gaza Jumatatu, kufuatia mivutano na watawala wanamgambo wa Hamas wa eneo hilo, maafisa walisema.

Ilikuwa mara ya kwanza kivuko cha Rafah kufungwa katika siku za kazi tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Mamlaka ya Misri ililiacha wazi eneo wakati wa siku 11 za vita kati ya Israel na Hamas hapo mwezi Mei.

Kulingana na maafisa wa Misri, kufungwa kwa eneo hilo kunahusishwa na juhudi za Cairo kusimamia sitisho la muda mrefu la mapigano kati ya Israel na hamas. Haikufahamiska mara moja eneo hilo litafungwa kwa muda gani, maafisa walisema.

Mmoja wa maafisa alisema hatua hiyo ililenga kuishinikiza Hamas, kwa sababu ya tofauti kati ya Cairo na kundi la wanamgambo kufuatia ukosefu wa maendeleo kwa wote yanayoongozwa na Misri, mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Israel, na pia juhudi za upatanshi na vikundi vya wapalestina. Maafisa walizungumza kwa sharti la kutotajwa majina kwa sababu hawakuruhusiwa kuzungumza na waandishi wa habari.

Kufungwa kwa eneo kumekuja saa kadhaa, baada ya shirika la habari la serikali ya Misri kuripoti kwamba sehemu ya kivuko ilifunguliwa jana Jumapili, baada ya kufungwa kwa wiki nzima kufuatia wikiendi ya waislam, Ijumaa na Jumamosi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG