Ethiopia inakaribia kukamilisha kujaza bwawa kubwa kwenye mto Blue Nile kwa mwaka wa pili, vyombo vya Habari vya serikali viliripoti Jumatatu hatua ambayo imeikasirisha Misri.
Addis Ababa inasema bwawa la Grand Renaissance (GERD) mradi wa umeme wa maji uliogharimu dola bilioni 4 ni muhimu kwa maendeleo yake ya kiuchumi na kusambaza umeme. Lakini limesababisha wasi wasi juu ya uhaba wa maji na usalama nchini Misri na Sudan ambao pia wanategemea maji ya mto Nile.
Ujazaji wa awamu ya pili wa bwawa la GERD utakamilika kwa muda mfupi shirika la utangazaji la Ethiopia liliripoti Jumatatu. Misri ilisema mwezi uliopita ilikuwa imepokea taarifa rasmi kutoka Ethiopia kwamba imeanza kujaza hifadhi kwa mara ya pili na alisema Ethiopia ilikataa hatua hiyo.
Misri inaiona hatua hiyo kama tishio kubwa kwa usambazaji wake wa maji ya Nile ambayo inayategemea kwa kiasi kikubwa. Sudan pia imeonyesha wasi wasi juu ya usalama wa bwawa na athari kwenye mabwawa yake mwenyewe na vituo vya maji.