Wawakilishi wa Afrika katika soka ya Olympiki Ivory Coast wamejiweka katika nafasi nzuri kuingia robo fainali baada ya timu hiyo kutoka sare ya bila kufungana na Brazil.
Timu ya Ivory Coast inahitaji sare tu kufuzu robo fainali ambapo ni timu mbili tu za juu kutoka kila kikundi watakaoingia.
Brazil ilicheza na wachezaji 10 tu kwa muda mwingi wa mchezo huo ambapo walitoka sare ya 0-0 Jumapili katika hatua ya makundi ya mashindano ya mpira wa miguu ya wanaume ya Olimpiki.
Nao mafarao wa Misri walijikuta katika wakati mgumu baada ya kushindwa na Argentina kwa bao 1-0 siku ya jumapili.
Kwa matokeo hayo sasa Misri watahitaji kuifunga Australia na kuomba Spain ishindwe na Argentina ili iweze kwenda robo fainali.
Wakati huo huo wana Bafana Bafana Afrika Kusini ambao walipoteza mchezo wao wa pili dhidi ya Ufaransa kwa magoli 4-3, wachezaji wao wawili walikumbwa na maambukizi ya Covid-19 katika Kijiji cha Olimpiki kabla ya mashindano kuanza, watahitaji kuifunga Mexico katika mchezo wao wa mwisho wa kundi A na wakitumai Japan iwafunge Ufaransa ili kuwa na nafasi yoyote ya kuingia robo fainali.
Nao wenyeji Japan wanaongoza kundi lao baada ya kushinda michezo yao miwili ya kwanza wakiwa na pointi 4 katika kundi A.