Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 25, 2024 Local time: 20:19

Mdahalo wa wagombea urais Uganda wasitishwa kwa muda usiojulikana

Mwanamuziki mashuhuri wa Uganda na mgombea urais Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, akimsaidia mlinzi wake aliyeumizwa katika ghasia zilizozuka kati ya wafuasi wa Wine na vikosi vya usalama huko Kayunga Kampala, Uganda, Disemba. 1, 2020.

Mdahalo wa siku mbili kwa ajili ya wagombea urais wa Uganda umefutwa kwa muda usiojulikana.

Baraza la ushirikiano wa kidini lililokuwa linaandaa mdahalo huo uliotarajiwa kuanza Ijumaa limesema uamuzi huo umetokana na ukosefu wa rasilimali, vyombo vya habari vimeripoti.

Baraza hilo pia limesema hali ya COVID – 19 imechangia pia kuahirishwa kwa mdahalo huo mnamo saa za mwisho.

Waandaaji wamedai kuwa mdahalo huo wa urais ulitarajiwa kuwakutanisha wagombea 10.

Wakati huo huo Kampeni zinaendelea nchini Uganda huku polisi mara kwa mara wakitawanya kundi kubwa la waandamanaji wanaoshutumiwa kwa ukiukwaji wa masharti yaliyowekwa na Tume ya Uchaguzi.

Mmoja wa wagombea urais Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine ametoa wito kwa tume ya uchaguzi kulinda wanasiasa wa upinzani dhidi ya manyanyaso ya maafisa wa usalama.

XS
SM
MD
LG