Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 13:39

Polisi Uganda yatangaza kuanza uchunguzi wa ghasia zilizo sababisha vifo 45


 Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine
Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine

Polisi nchini Uganda imeanza kufanya uchunguzi wa ghasia za ukandamizaji dhidi ya waandamanaji wiki iliyopita zilizo sababisha vifo vya takriban watu 45, gazeti la Uganda la 'Daily Monitor' limeripoti.

Msemaji wa polisi Fred Enanga amesema uchunguzi huo unazingatia zaidi makosa yaliyo sababisha uharibifu.

Wajumbe wa Umoja wa Ulaya tayari wametoa wito wa kufanywa uchunguzi huru zaidi, kutokana na vitendo vya polisi dhidi ya waandamanaji ili kuhakikisha sheria inafuata mkondo wake kwa walioathiriwa na kuepuka kutohukumiwa waliohusika na ukatili ambao ni lazima wachukuliwe hatua.

Wiki iliyopita polisi walionekana wakitumia nguvu na silaha wakati wakipambana na waandamanaji waliokuwa wanalalamika dhidi ya kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani Robert Chagulani maarufu kama Bobi Wine.

Bobi Wine alishtakiwa kwa kukiuka masharti ya kupambana na kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona. Mwana siasa huyo aliachiwa huru kwa dhamana na anaendelea na kampeni zake.

XS
SM
MD
LG