Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 19:33

Uganda imepata 'dawa ya Corona'. Majaribio yamefaulu kwa watu kadhaa


Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kwamba wanasayansi nchini humo wamepiga hatua kubwa sana katika kupata tiba dhidi ya Corona.

Katika hotuba kwa taifa jana jumapili, Museveni amesema kwamba wanasayansi nchini humo wamefanyia majaribio tiba hiyo ambayo hakutoa maelezo zaidi, akiongezea kwamba kwa sasa, madaktari wanatumia mchanganyiko wa vitu maalum ambavyo vinaongeza kinga mwilini dhidi ya virusi vya Corona.

“wanasayansi wetu wameniambia habari njema kwamba wameunda dawa saba tofauti. Sita kati ya hizo zinafanyiwa majaribio na moja inaongeza kinga ya mwili dhidi ya virusi vya Corona.” Amesema Museveni katika hotuba iliyopeperushwa na runinga zote za habari nchini Uganda, akiongezea kwamba “dawa za kwanza tatu zinauwa virusi hivyo na kuzuia uharibifu mwilni.”

Museveni amesema kwamba dawa hiyo imefanyiwa “majaribio kwa wagonjwa kadhaa wa Corona na kupona na itaanza kutumika vikamilifu kwa watu wote Desemba tarehe 15 mwaka huu.”

Ameendela kusema kwamba “katika mda wa siku 40, dawa hiyo itakuwa imetibu watu wengi na kuweka Imani kati yaw engine kwamba inaweza kutibu Corona na virusi vingine.”

Museveni ameongezea kusema kwamba “wanasayansi wa Uganda wamezindua vipimo vya Corona kwa kuumia sampuli ya mate na kutoa matokeo ndani yam da wa dakika 30.”

Jumla ya watu 210 wamefariki kutokana virusi vya Corona nchini Uganda.

Kampuni kadhaa nchini Marekani na ulaya zimetangaza kupata chanjo dhidi ya virusi vya Corona.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG