Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Agosti 03, 2021 Local time: 16:00

Rais Museveni anukuu Bibilia katika ujumbe mzito kwa upinzani


Rais wa Uganda Yoweri Museveni aiwasili katika mkutano wa nchi za Umoja wa Africa (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia, Feb. 9, 2020.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni siku ya Jumapili alijigamba juu ya nguvu za kijeshi na alionekana kutishia upinzani. Akirejelea mapigano ya usalama kwenye maandamano ya upinzani mwezi huu ambayo yalisababisha vifo vya watu 54, Museveni alinukuu Bibilia, akisema wakosaji wanastahili kifo.

Katika hotuba maalum, Rais Yoweri Museveni, ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 34, alivaa koti la kijeshi na hakumumunya maneno. Akirejelea vyama vya upinzani kama "magenge ya wahalifu", Museveni alisema maandamano ya vurugu ambayo yalisababisha kupoteza maisha ya watu 54 hayatarudiwa kamwe.

Wakati wa hotuba hiyo, alipitia video za waandamanaji wanaoharibu magari na mabango yake ya kampeni na kumvua nguo mwanamke ambaye alikuwa amevalia fulana ya manjano.

Aliviita vitendo hivyo ni wafuasi wa upinzani kupata msaada wa nje na kutokuhofia kushtakiwa.

Museveni, ambaye pia ni mkuu wa vikosi vya ulinzi, anasema majibu dhaifu ya polisi katika siku za nyuma yamepelekea maoni potofu kwamba usalama wake pia ni dhaifu.

“Kwa kweli ilikuwa hesabu potofu kwa matapeli kufikiria kwamba wanaweza kutumia mbinu kama hizi za kupambana na watu katika nchi inayoongozwa na Jeshi la Awali la Upinzani la Kitaifa. Hali nzima ya usalama wa Uganda ni thabiti. Huna haki ya kuwapiga mawe Waganda na kuwavua nguo ikiwa ni pamoja na wanawake, kwa sababu tu wamevaa mavazi ya manjano. Huna haki ya kuharibu mali.”alisema.

Kuhusu video za wanajeshi wanaowapiga risasi raia, alisema zitachunguzwa na kwamba ufafanuzi wa kwanini hawakupiga risasi hewani utatolewa.

Museveni alisema kati ya wale 54 waliouawa, 20 hawakuwa waandamanaji na kwamba watalipwa fidia.

Akinukuu Biblia, Museveni alikuwa na yafuatayo kuwaambia wafanya ghasia na wafuasi wao:

“Katika kitabu cha Warumi Sura ya Kwanza, Mstari wa 32, inasema,

Ingawa wanafahamu sheria ya haki ya Mungu kwamba watu wanaofanya mambo kama hayo wanastahili mauti, si kwamba wanaendelea kutenda hayo tu, bali pia wanakubaliana na wale wanaoyatenda.”

Museveni alisema chama cha upinzani cha National Unity Platform, kinachoongozwa na Bobi Wine, na chama cha Forum for Democratic Change, kinachoongozwa na Amuriat Patrick Oboi, wanadhani hawawezi kuguswa na watashughulikiwa.

Ssemujju Ibrahim Nganda, msemaji wa FDC, anasema ujumbe wa Museveni kwa upinzani ni kwamba wao na wafuasi wao wako hatarini.

Waganda wanakwenda kwenye uchaguzi Januari 14 kumchagua rais wao ajaye.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG