Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:29

Mawaziri wakuu wa zamani Guinea-Bissau kushiriki duru ya pili uchaguzi


Uchaguzi Guiné-Bissau, 2019
Uchaguzi Guiné-Bissau, 2019

Mawaziri wakuu wawili wa zamani nchini Guinea-Bissau wamepita kushiriki duru nyingine ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

Mawaziri hao wanaingia katika kinyang'anyiro hicho baada ya kupata kura za kutosha katika kura zilizopigwa November 24, tume ya taifa ya uchaguzi imetangaza.

Domingos Simoes Pereira amekuwa wa kwanza kwa kupata asilimia 40, na Umaro Cissoko Embalo amekuwa wa pili kwa kupata asilimia 28 ya kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi, kwa mujibu wa rais wa tume ya uchaguzi Jose Pedro Sambu.

Viongozi hao watashindana katika duru nyingine ya uchaguzi uliopangwa kufanyika Desemba 29, 2019. Rais aliyekuwa madarakani José Mário Vaz, ametawala toka mwaka 2014.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa tume ya taifa imesema kwamba rais aliyepo madarakani ambaye alitetea kiti chake alishika nafasi ya nne kwa kupata asilimia 12 ya kura zote zilizopigwa.

Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa inadaiwa utawala wake umekumbwa na kashfa za rushwa.

XS
SM
MD
LG