Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 15:19

Ghasia zafuatia kujiuzulu kwa Rais wa Bolivia


Wapinzani wa Rais wa zamani wa Bolivia wameshika ngao wakiwa wamezingira kasri ya rais huko Pa Paz.
Wapinzani wa Rais wa zamani wa Bolivia wameshika ngao wakiwa wamezingira kasri ya rais huko Pa Paz.

Ghasia na hali ya wasiwasi imeendelea kujitokeza nchini Bolivia Jumatatu kufuatia uamuzi wa Rais Evo Morales kujiuzulu kutokana na shinikizo la wananchi na vurugu za karibu wiki tatu.

Morales alisema : "Kaka na dada zangu nchini Bolivia na ulimwenguni kote, nawafahamisha niko hapa na Makamu wa Rais na Waziri wa Afya, na baada ya kuwasilikiliza rafiki zangu kutoka shirikisho la vuguvugu la kijamii na shirikisho la umoja wa kibiashara na pia kwa kusikiliza Kanisa Katoliki, natangaza kujiuzulu wadhifa wangu wa urais."

Uamuzi wa kiongozi wa chama cha kisoshalisti kujiuzulu kimefuatia muda mfupi tu baada ya kutangaza kwamba ataitisha uchaguzi mkuu mpya baada ya Jumuia ya Mataifa ya Amerika OAS kutangaza kwamba kulikuwepo na kasoro katika uchaguzi wa Oktoba 20.

Hali ya kutoelewana na wizi umetokea kutokana na kwamba haijulikani wazi nani atachukuwa nafasi ya kiongozi huyo aliyekuwa madarakani kwa muda wa miaka 14.

Marais Miguel Diaz Canel wa Cuba na Nicolas Maduro wa Venezuela wameeleza kumuunga mkono Morales wakieleza tukio hilo la Bolivia kama mapinduzi.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG