Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 12, 2024 Local time: 02:55

Upinzani Venezuela washinikiza Rais Maduro atengwe


Juan Guaido, mkuu wa upinzani walio wengi katika bunge la Venezuela ajitangaza rais wa muda mpaka uchaguzi utakapo fanyika na anashinikiza Rais Nicolas Maduro ajiuzulu huko Caracas, Venezuela, Jan. 23, 2019.
Juan Guaido, mkuu wa upinzani walio wengi katika bunge la Venezuela ajitangaza rais wa muda mpaka uchaguzi utakapo fanyika na anashinikiza Rais Nicolas Maduro ajiuzulu huko Caracas, Venezuela, Jan. 23, 2019.

Chama cha upinzani nchini Venezuela Alhamisi kimeendelea kushinikiza Rais Nicolas Maduro anayekabiliwa na utata wa kunang'ania madaraka atengwe, wakati idadi ya nchi kadhaa zinaongezeka zikitangaza kuwa zinamuunga mkono kiongozi wa muda Juan Guaido.

Guaido, spika wa Bunge la Venezuela, alijitangaza mwenyewe kuwa rais wa muda siku moja kabla, wakati wa maandamano makubwa.

Sakata hilo katika nchi hiyo ya Amerika Kusini lilizidi kuongezeka Jumatano baada ya Rais Maduro kutangaza kuwa anasitisha mahusiano ya kidiplomasia na Marekani, akijibu tangazo la Rais Donald Trump kwamba anamtambua rasmi Guaido kuwa ni Rais wa muda wa Venezuela.

Maduro ameamrisha kuwa wafanyakazi wote wa Ubalozi wa Marekani waondoke nchini katika kipindi cha masaa 72. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, hata hivyo, amesema Maduro hana tena madaraka ya kutoa amri hiyo.

Trump amemuonya Maduro kuwa “hatua mbalimbali tayari ziko mezani” kama hapatakuwa na kukabidhiana madaraka kwa amani ikiwa ni hatua ya kidemokrasia katika nchi hiyo ya Amerika Kusini.

Maafisa wa White House wanasisitiza kuwa Trump hajakanusha hatua ambazo anaweza kuchukua kama vile kuweka manuari ya kivita katika eneo hilo kuzuia harakati za nchi hiyo au kuchukua hatua nyingine za kijeshi, iwapo Maduro ataanzisha mashambulizi yeyote dhidi ya waandamanaji au kuchukua hatua dhidi ya Guaido.

Pengine hatua ya haraka zaidi itakayo chukuliwa na Washington ni kuendeleza vikwazo zaidi dhidi ya maafisa wa serikali ya Maduro.

XS
SM
MD
LG