Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 09, 2022 Local time: 08:07

Marekani imeishutumu Russia kupeleka ndege za vita Venezuela


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo

Kremlin ilijibu maoni ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo na kuyaita hayakubaliki na sio ya kidiplomasia hata kidogo kwa Pompeo kufanya hivyo

Marekani imeishutumu vikali Russia kwa kupeleka ndege mbili za kivita kwenda Venezuela kwa michezo ya vita. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo aliandika kwenye mtandao siku ya Jumanne kuwa watu wa Russia na Venezuela kwa nini waone michezo hii, serikali mbili zilizojaa rushwa zinatumia hovyo pesa za umma na kukandamiza uhuru wakati watu wao wanapata taabu.

Kremlin ilijibu maoni ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo na kuyaita hayakubaliki na sio ya kidiplomasia hata kidogo kwa waziri huyo kufanya hivyo.

Msemaji wa Russia, Dmitry Peskov
Msemaji wa Russia, Dmitry Peskov

Msemaji wa Russia Dmitry Peskov alisema Marekani haina sababu ya kukosoa fedha zinazotumika kwa mazoezi akisema ni nusu ya bajeti ya ulinzi ya Marekani ambayo inaweza kulisha watu barani Afrika.

Ndege mbili za Russia zina uwezo wa kubeba silaha za nyuklia ambazo zilitua Venezuela siku ya Jumatatu kwa kile ambacho maafisa wa Venezuela walisema ni mazoezi ya kijeshi ambayo yalipangwa kuboresha uwezo wao wa ulinzi. Russia imepeleka marubani 100 na wanajeshi wengine.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG