Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 14:28

Kampeni za urais Algeria zimeanza rasmi Jumapili


Mmoja wa wagombewa wa urais Algeria, Abdelmadjid Tebboune
Mmoja wa wagombewa wa urais Algeria, Abdelmadjid Tebboune

Mawaziri wa zamani wawili huko Algeria, Ali Benflis na Abdelmadjid Tebboune ni miongoni mwa wagombea katika uchaguzi utakaofanyika Disemba 12 wa kuchukua nafasi ya rais wa zamani nchini humo Abdelaziz Bouteflika

Kampeni za urais Algeria zimeanza rasmi Jumapili kwa wagombea watano kila mmoja ana nia ya kuchukua nafasi ya kiongozi wa muda mrefu aliyeondolewa madarakani mwezi April, Abdelaziz Bouteflika kufuatia maandamano ya muda mrefu.

Mawaziri wa zamani wawili huko Algeria, Ali Benflis na Abdelmadjid Tebboune ni miongoni mwa wagombea katika uchaguzi utakaofanyika Disemba 12 wa kuchukua nafasi ya rais wa zamani nchini humo Abdelaziz Bouteflika.

Umati mkubwa uliingia mitaani Ijumaa kwa wiki ya 39 mfululizo wakidai kikomo cha mfumo wa kisiasa baada ya ukoloni nchini Algeria. Waandamanaji walisema hawana imani na watu waliopo hivi sasa madarakani kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa kidemokrasia, wakielezea uhusiano wa watu hao na kiongozi wa zamani nchini humo Bouteflika.

Benflis na Tebboune ndio wagombea wanaopewa kipaumbele kwenye upigaji kura.

XS
SM
MD
LG