Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 26, 2022 Local time: 12:07

Kiongozi wa upinzani Bolivia atangaza kuwa rais wa muda


Senata Jeanine Anez akiwa katika kasri ya rais huko La Paz, Bolivia, Nov. 12, 2019.

Kiongozi wa upinzani katika baraza la senate nchini Bolivia amejitangazia kuwa ni Rais wa muda Jumanne baada ya kujiuzulu kwa kiongozi wa zamani Evo Morales.

Jeanine Anez mwenye umri wa miaka 52 alichukuwa udhibiti wa baraza la senate Jumanne na kujiweka katika nafasi ya kuwa rais ajaye.

Wabunge wa chama cha Morales, Movement for Socialism walikuwa hawako bungeni wakati Anez alipotoa tangazo hilo.

Morales aliachia madaraka Jumapili kwa pendekeo la mkuu wa jeshi nchini humo kufuatia wiki kadhaa za maandamano tangu uchaguzi uliokuwa na utata ambao ulimrejesha madarakani kwa awamu ya nne.

Maelfu ya wafuasi wa Rais wa zamani Morales ambaye hivi sasa anaishi uhamishoni waliingia mitaani katika mji mkuu wa Bolivia.

Waandamanaji wanaamini kuondolewa kwa Morales ni mapinduzi napia ni kitendo cha ubaguzi dhidi ya jamii za wazawa nchini Bolivia. Licha ya ghadhabu zao, maandamano yalikuwa ya amani.

Nje ya mji mkuu, polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kwa kupambana na wafuais wa Morales katika mji wa Cochabamba.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG