Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:45

Watu 76 wafariki katika ajali ya ndege Colombia


wachezaji wa timu ya Chapecoense kabla ya kuelekea katika michuano ya Copa Amerika ya kusini kupambana na timu ya Argentina ya San Lorenzo in Buenos Aires, Argentina, Nov. 2, 2016.
wachezaji wa timu ya Chapecoense kabla ya kuelekea katika michuano ya Copa Amerika ya kusini kupambana na timu ya Argentina ya San Lorenzo in Buenos Aires, Argentina, Nov. 2, 2016.

Brazil imetangaza siku tatu za maombolezi ya kitaifa kufatia ajali ya ndege iliyokua inasafirisha timu ya kandanda ya mji wa Chapeco, Brazil kuelekea Medellin, Colombia, Juamtatu usiku, ili kushiriki katika finali ya kombe la klabu bingwa ya Amerika Kusini, COPA.

Maafisa wa usalama wanasema watu watano kati ya 81 walokua ndani ya ndege hiyo walinusurika katika ajali iliyotokea Medellin.

Ndege hiyo iliyokodishwa kutoka kampuni ndogo ndege ya Venezuela, LaMia ilikua inasafiri kutoka mji wa Santa Cruz, Bolivia, kuelekea Medellin Colombia, iliripoti kua ina matatizo ya umeme muda mchache kabla ya kuanguka.

Timu iliyokua inasafiri katika ndege hiyo ya Chapocoense, ni timu ya division ya kwanza kutoka mji wa kusini ya Brazil wa Chapeco, na ilipangwa kucxheza mchezo wao wa kwanza siku ya Jumatano katika finali ya COPA.

Rais wa Brazil Michael Temer amesema maafisa wa serikali watafanya kila wawezalo kusaidia timu hiyo na familia zao pamoja na waandishi habari walofariki kwenye ajali hiyo.

XS
SM
MD
LG