Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 17:10

Moto waendelea kuteketeza msitu mkubwa duniani wa Amazon


Moshi katika msitu wa Amazon karibu na mji wa Humaita katika jimbo la Amazonas, Brazil, Agosti 14, 2019.
Moshi katika msitu wa Amazon karibu na mji wa Humaita katika jimbo la Amazonas, Brazil, Agosti 14, 2019.

Bolivia imetoa wito uwepo ushirikiano wa nchi tatu, utakaohusisha Brazil na Paraguay, kuzima moto unaoendelea kuteketeza kwa kasi msitu mkubwa dunani wa Amazon uliopo kati ya nchi hizo tatu.

Maafisa katika mkoa wa Santa Cruz, wanakadiria kwamba moto huo uliyoenea maeneo mbali mbali, mashariki mwa Bolivia, tayari umekwisha teketeza zaidi ya hekta 450,000.

Jeshi la Bolivia linaendelea na juhudi za kuzima moto huo ambao umefikia sehemu ya daraja la Rio Negro, kati ya miji ya Puerto Suarez na Puerto Busch, mpakani mwa Brazil, Paraguay na Bolivia.

Waziri katika ofisi ya Rais wa Bolivia Huan Ramon Quintana, ametoa wito wa ushirikiano kuzima moto huo huku maelfu ya mioto mingine ikiwa inaendelea kuteketeza msitu huo wa Amazon.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG