Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 11:12

Ajali ya Moto : Wafanyabiashara wapoteza mali zao Mwanza


Tanzania
Tanzania

SOKO la wafanyabiashara wa nguo na viatu mjini Mwanza, Tanzania, limefungwa Jumamosi kwa muda wa siku mbili baada ya kuteketea kwa moto majira ya saa 10:00 alfajiri .

Moto uliounguza soko hilo, maarufu kama Soko la Mlango Mmoja, ambalo liko Kata ya Mbugani, Wilaya ya Nyamagana, unadaiwa kuwa huenda chanzo chake ni majiko yakiwa na moto yaliyo telekezwa katika eneo hilo.

Vyanzo vya habari vimesema kuwa soko hilo lina zaidi ya wafanyabiashara 1,000 na linategemewa na wafanyabiashara wa mkoa wa Mwanza.

Zaidi ya maduka 150 na vibanda 100 pamoja na mali zilizo kuwamo katika eneo hilo, vimeteketea kwa moto na kusababishia hasara kubwa.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, alitembelea soko hilo na kuwaelekeza viongozi wa mitaa na wilaya ya Nyamagana washirikiane na viongozi wa soko ili kuweka utaratibu mzuri wa kutambua vitu.

"Mtangaze kufunga soko kwa siku mbili na ikiwezekana soko lirekebishwe sehemu ambayo haikuungua hadi Jumatatu shughuli zitakapoanza ili kwa hizi siku za kufungwa kwa soko viongozi wakae ili kubaini hatua gani za awali zichukuliwe," alisema Mongella.

Naye Kamamda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna alisema walifanikiwa kuudhibiti moto huo kwa asilimia 95 na kwamba chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.

" Ingawa kuna tetesi kuwa inawezekana ikawa ni hawa ndugu zetu wanao jishughulisha na kazi ya kunyoosha nguo au mama ntilie, lakini natoa onyo kwa watu wanaoitwa vibaka wasijaribu kufanya harakati zozote za wizi, msithubutu kuiba chochote atakaye thubutu atabadilika kuwa majivu," alisema Shanna.

XS
SM
MD
LG