Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 29, 2022 Local time: 07:12

Tanzania : Mazishi ya wahanga wa MV Nyerere yafanyika kitaifa


Shughuli za uchunguzi zikiendelea katika eneo la ajali ambako Ferri - MV Nyerere ilizama.

Ibada ya mazishi ya kitaifa nchini Tanzania ya baadhi ya watu walio poteza maisha katika ajali ya Ferri - MV Nyerere iliyozama Septemba 20, 2018 yamefanyika Jumapili.

Mazishi hayo yamefanyika katika kijiji cha Bwisya, Kisiwa cha Ukara, Wilaya ya Ukerewe, Mkoa wa Mwanza, na kuongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Mazishi hayo yalihudhuriwa na viongozi wengine ambao wapo kisiwani hapa kushiriki mazishi ya miili ambayo haijatambulika na ambayo ndugu wameomba izikwe kwa utaratibu ulioandaliwa na Serikali.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari miili 224 imeopolewa, 172 kutambuliwa na 112 imekabidhiwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi. Hadi sasa miili 37 haijaweza kutambuliwa.

Zoezi la ukoaji linaendelea wakati mazishi yataendelea kufanyika pale miili ikipatikana na Waziri mkuu ataendelea kubaki kisiwani Ukara.

Wakati huo huo serikali imeunda tume ya uchunguzi itakayo husisha timu ya wataalamu na vyombo ya dola, kuhakikisha chanzo cha ajali kinatambulika.

Kwa upande wake Waziri wa Uchukuzi mhandisi Isack Kamwelwe amesema kuwa jumla ya miili 224 imeopolewa.

Taarifa zinasema kuwa maafisa wote wanao husika na uendeshaji wa kivuko wamekamatwa na wanahojiwa kwa uchunguzi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG