Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 27, 2023 Local time: 03:48

MV Nyerere : Mtu mwengine aokolewa, walio kufa wafikia 207


Waokoaji nchini Tanzania wakiopoa miili ya wahanga waliokufa katika ajali ya Ferri - MV Nyerere, Ziwa Victoria, Tanzania, Septemba 22, 2018.

Wapiga mbizi Jumamosi wamemuokoa mtu mmoja kutoka katika mabaki ya Ferri-MV Nyerere iliyokuwa imezama Ziwa Victoria, Mkoa wa Mwanza, nchini Tanzania, Alhamisi, na hadi sasa watu wasio pungua 207 wamepoteza maisha.

Shirika la habari la Reuters linaripoti kuwa miili iliendelea kuelea kuzunguka chombo hicho, ambapo hapo awali ilikuwa imekadiriwa kuwa ferri hiyo ilikuwa imebeba watu zaidi ya 300.

Kituo cha Televisheni cha Taifa TBC kimetangaza kuwa idadi ya walioopolewa imefikia miili 207.

Wazamiaji wa jeshi la majini nchini waliendelea kutafuta miili ndani ya ferri- MV Nyerere mapema Jumamosi baada ya kusikia sauti ambazo ziliashiria wapo watu walio kuwa bado hai.

Waliweza kuuopoa mtu mmoja kutoka katika ferri hiyo iliyobinuka na mara moja kupelekwa hospitali, aliyeshuhudia hilo ameliambia Shirika la Reuters, Hali ya mtu huyo haijulikani ikoje.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG