Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 12:43

Moto Uingereza: Nyumba 20 zateketea mashariki ya London


Jengo lilioko Natalie Oxford likiwaka moto on Juni 14, 2017, upande wa magharibi ya London.
Jengo lilioko Natalie Oxford likiwaka moto on Juni 14, 2017, upande wa magharibi ya London.

Nyumba 20 ziliteketezwa na moto na nyingine 10 zimeharibiwa baada ya moto kushika jengo moja huko mashariki ya London.

Moto huo ulienea katika ghorofa zote sita katika jengo hilo katika eneo la De Pass Gardens, Barking, majira ya saa tisa na nusu mchana majira ya Uingereza, ofisi ya zimamoto London imesema.

Takriban wazimamoto 100 walifanya kila wawezalo kwa zaidi ya masaa mawili kuzima moto huo, ambao hatimaye ulizimwa majira ya saa kumi na mbili jioni. Chanzo cha moto huo bado kinafanyiwa uchunguzi.

Mtu mmoja na mwanamke mmoja walitibiwa kwa kuathiriwa na moshi waliokuwa wanauvuta wakati ajali hiyo ya moto ilipotokea.

Wawili hao walipatiwa matibabu katika eneo la ajali na hakuna taarifa nyingine juu ya majeruhi.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington DC

XS
SM
MD
LG