Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 26, 2023 Local time: 05:32

Mashirika ya ndege yapata hasara kutokana na mgomo Kenya


Wafanyakazi wa shirika la ndege la Kenya wakitawanywa na askari wa kikosi cha kuzuia ghasia katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta International Airport,Nairobi, Kenya, March 6, 2019.

Wasafiri nchini Kenya iliwabidi wasubiri kwa muda mrefu wakati mashirika ya ndege na biashara zikihisabu hasara kubwa kutokana na mgomo wa wafanyakazi uliyosimamisha operesheni za viwanja vya ndege Jumatano.

Athari za hasara ya fedha zinazotokana na vitendo hivi vya uvunjaji sheria ni kubwa. Bado tunafanya mahesabu na tutatoa kiwango halisi cha hasara hii

"Kufutwa au kubadilishwa kwa safari za ndege huja na gharama ikiwemo kuwarejeshea abiria nauli zao, kuwapa malazi abiria waliokwama, siyo tu hapa Kenya lakini katika viwanja vingine vya ndege ambapo ndege zao zilikuwa zimalize safari Nairobi. Hili litasababisha hasara isiyokifani kwa mashirika ya ndege," Waziri wa Usafiri James Macharia amesema.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa KQ Sebastian Mikosz amesema bado hawajamaliza kufanya mahesabu ya hasara iliyopatikana kwa shirika la ndege hilo, lakini katika makaratasi waliopeleka mahakamani kufungua shauri hilo Jumatano asubuhi, shirika hilo limeonyesha hasara iliyotokana na mgomo huo kuwa ni Shilingi milioni 300 za Kenya (dola milioni 3).

Wanachama wa jumuiya ya wafanyakazi wa viwanja vya ndege walikuwa wanapinga pendekezo la kuunganisha shirika la ndege la taifa la Kenya Airways na wasimamizi wa viwanja hivyo, na kama ikipitishwa, itaifanya KQ kuendesha viwanja hivyo kwa mkataba wa gharama nafuu wakishirikiana na Mamlala ya viwanja vya ndege Kenya (KAA).

Ndege zilizokuwa zifanye safari hazikuondoka na hakuna ndege iliyotuwa uwanja wa JKIA hadi majira ya saa tano asubuhi saa za Afrika Mashariki, wakati shirika la ndege la Rwanda ambalo lilikuwa limepangiwa kuchukuwa abiria kuondoka ikiwa tupu.

Abiria wengi walikuwa wakizunguka uwanja wa ndege wakisubiri kujua hatima ya safari zao, wakati serikali ilipoamrisha Jeshi la Wananchi la Kenya (KDF) kuendesha shughuli za uwanja wa ndege katika eneo la kutua na kuruka ndege.

KQ ilipata hasara kubwa kuliko zote katika masaa 24 yalioathiri ndege zake na bado ilikuwa inafanya juhudi za kuanza safari zake ili kukidhi mahitaji ya abiria ambao walikuwa wamekwama uwanjani hapo.

JKIA inapokea kwa wastani abiria 13,000 kila siku, na zaidi ya abiria 8,000 huanza safari zao kutoka katika uwanja huu.

Uwanja wa ndege huu ambao ni kiunganishi kwa mashirika mengi ya ndege unashughulikia kwa wastani ndege 230 kwa siku, na takriban ndege 114 zikiondoka kwa ajili ya safari za ndani ya nchi, kikanda na kimataifa.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG