Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 01:32

Marekani yamuwekea vikwazo kaka wa Jenerali ‘Hemedti’ Sudan


Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo wa Kikosi cha Msaada wa Dharura (RSF) akiwahutubia wafuasi huko Khartoum, Juni 20 2019. Picha na REUTERS/Umit Bektas.
Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo wa Kikosi cha Msaada wa Dharura (RSF) akiwahutubia wafuasi huko Khartoum, Juni 20 2019. Picha na REUTERS/Umit Bektas.

Marekani inamuwekea vikwazo naibu kiongozi wa Kikosi cha Msaada wa Dharura cha Sudan (RSF) kutokana na ukiukaji wa haki za binadamu, mjumbe wa Marekani katika Umoja wa Mataifa atatangaza wakati wa safari yake kwenye mpaka wa Chad na Sudan siku ya Jumatano.

Hatua hii inamlenga Abdelrahim Dagalo – kaka yake kamanda Mohamed Hamdan Dagalo ambaye ni kiongozi wa RSF, anayejulikana kama ‘Hemedti’ – amekuwa kiongozi wa ngazi ya juu kuwekewa vikwazo tangu mzozo kati ya kikosi cha RSF na jeshi la Sudan ulipozuka katikati ya mwezi wa Aprili na ikiwa ni majibu ya dhahiri kwa ghasia kubwa zilizoonekana huko Darfur Magharibi, ambapo vikosi vya RSF pamoja na washirika wanamgambo wanashutumiwa kwa ghasia hizo.

RSF imekanusha shutuma zinazotolewa na wachunguzi wa migogoro, vikundi vya kutetea haki za binadamu na mashahidi kwamba RSF imehusika na ghasia hizo, wakati wakisema hakuna mwanajeshi wake yeyote ambaye atakayebainika kuhusika na vitendo hivyo atafikishwa mahakamani.

Dagalo ni afisa wa kwanza kuwekewa vikwazo tangu vita vizuke. Vikwazo vya awali, Vikwazo vya awali vililenga makampuni, pia na jeshi.

Afisa huyo wa kijeshi amewekewa vikwazo "kwa kuhusika kwake na ukiukaji uliokuwa ukifanywa na RSF dhidi ya raia nchini Sudan, ikiwemo manyanyaso ya kingono na mauaji ya kikabila," Linda Thomas-Greenfield atawaambia waandishi wa habari, kulingana na maandishi yaliyotayarishwa ambayo shirika la habari la Reuters imeyaona.

Thomas-Greenfield anatoa tangazo hilo baada ya kukutana na wakimbizi wa Sudan ambao wamekimbia hali mbaya ya migogoro ya kikabila na kingono katika jimbo la Darfur nchini Sudan, ambapo alilielezea kuwa "inakumbusha" ukatili uliofanywa miaka 20 iliyopita huko Darfur, ambao Washington ilitangaza kuwa ni mauaji ya kimbari.

Waathirika wa ghasia wanaelezea kuwa ghasia hizo ziliwalenga watu wa kabila Masalit, pamoja na uharibifu wa vitongoji, uporaji ulioenea na ubakaji ambao umewalazimisha maelfu ya watu kukimbilia nchini Chad. The Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu imetangaza uchunguzi kuhusu ghasia hizo.

Vita vilizuka nchini Sudan Aprili 15, miaka minne baada ya rais wa zamani Omar al-Bashir kuondolewa madarakani na uasi wa wananchi. Mivutano kati ya jeshi (SAF) na RSF, ambao kwa pamoja walifanya mapinduzi mwaka 2021, na hatimaye vita kuzuka wakipigana juu ya mpango wa mpito wa utawala wa kiraia unaoungwa mkono kimataifa na kuunganisha vikosi vyao.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG