Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 12:55

Utawala wa Biden kuongeza muda na kuibadilisha programu inayowapa hifadhi raia wa Sudan na Ukraine


FILE PHOTO: U.S. President Joe Biden speaks about recovery efforts in Maui, Hawaii, and the ongoing response to Hurricane Idalia, in Washington
FILE PHOTO: U.S. President Joe Biden speaks about recovery efforts in Maui, Hawaii, and the ongoing response to Hurricane Idalia, in Washington

Utawala  wa Rais Biden hivi karibuni umetangaza kuongeza muda na kuibadilisha tena programu inayowapa hifadhi ya muda raia wa Sudan na Ukraine ili kutokuondolewa nchini Marekani. Raia wa El Salvador, Honduras, Nepal na Nicaragua pia hifadhi yao imeongezwa muda.

Programu hiyo inayojulikana kama Temporary Protected Status (TPS) inawaruhusu wahamiaji ambao nchi zao zinachukuliwa kuwa siyo salama, wanaruhusiwa kuishi na kufanya kazi nchini Marekani kwa kipindi fulani iwapo watakidhi vigezo vilivyowekwa na serikali ya Marekani.

Katika matamshi yake Jumatano na waandishi, mawakili wa uhamiaji waliusihi utawala wa Biden kuziingiza nchi mpya katika hadhi hiyo ya TPS na kuzibadilisha zilizokuwepo katika hadhi hiyo ili kuwaruhusu watu zaidi kufikia viwango vya programu hiyo ili waweze kufanya kazi kihalali nchini Marekani.

Daniel Costa, mkurugenzi wa utafiti wa sheria ya uhamiaji na sera katika Taasisi ya Sera ya Uchumi, alisema wale wenye vibali vya TPS hivi sasa wana viwango vya juu vya ushiriki wa nguvu kazi na wanachangia mabilioni katika uchumi wa Marekani kila mwaka.

“TPS inaongeza kipato cha watu kupitia ruhusa iliyopo ya kufanya kazi kwa watu wasiokuwa na kazi. … Kipato cha juu pia kinamaanisha ni matumizi yanayorejea katika uchumi huo, ambao unatengeneza ajira zaidi,” alisema.

Muundo wa TPS wa awali kwa watu wa Honduras, Nicaragua na El Salvador ulitengenezwa zaidi ya miaka 20 iliyopita. Wakati uongozi wa Biden ulipoongeza muda wa TPS kwa nchi hizo mwezi Juni, ilikuwa kwa ajili ya waliokuwa na hadhi hiyo hivi sasa.

Iwapo utawala wa Biden utaitengeneza tena TPS, itabadilisha tarehe ya mwisho ambayo watu walitakiwa waingie Marekani ili kuweza kufikia kiwango cha programu hiyo, na wale walioingia katika kipindi cha miaka 20 watakuwa wanastahiki.

Kulingana na ripoti ya Kituo cha Niskanen, taasisi ya utafiti wa sera yenye makao yake Washington, “wengi wao wenye vibali vya TPS wameajiriwa.

Vyanzo vya habari hii ni mashirika ya habari ya Reuters, AP na AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG