Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 12, 2024 Local time: 02:41

Jumuia ya nchi za Afrika ya kati yalaani mapinduzi nchini Gabon


Kanda ya video ikionyesha wanajeshi wakimnyanyua juu kiongozi wa mapinduzi Jenerali Brice Oligui Nguema mjini Libreville, Gabon Agosti 30, 2023.
Kanda ya video ikionyesha wanajeshi wakimnyanyua juu kiongozi wa mapinduzi Jenerali Brice Oligui Nguema mjini Libreville, Gabon Agosti 30, 2023.

Jumuia ya nchi za Afrika ya Kati ECCAS Alhamisi imelaani matumizi ya nguvu kutatua mzozo wa kisiasa nchini Gabon na kuomba utaratibu wa kikatiba urejeshwe haraka nchini humo.

Jumuiya hiyo ya uchumi ya nchi za Afrika ya Kati imesema katika taarifa kwamba imekuwa ikifuatilia kwa karibu hali nchini Gabon, na kwamba wakuu wa nchi hizo watafanya mkutano wa dharura kujadili hali ya kisiasa na kiusalama nchini humo.

Baada ya maafisa wa jeshi kuchukua madaraka na kumuweka Rais Ali Bongo katika kizuizi cha nyumbani siku ya Jumatano, mataifa mengine yalilaani matukio hayo, ikiwemo Marekani ambayo iliomba Bongo aachiwe huru na kuendelezwa kwa utawala wa kiraia.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Matthew Miller alisema katika taarifa “Marekani ina wasiwasi mkubwa na matukio yanayoendelea nchini Gabon. Amesema wanaendelea kupinga vikali jeshi kunyakua madaraka na kukabidhiana madaraka kinyume cha katiba.

Miller alibaini pia wasiwasi kuhusu “ukosefu wa uwazi na ripoti za kasoro zilizogubika uchaguzi nchini Gabon ambapo Bongo alishinda muhula wa tatu madarakani.

Wanajeshi walioasi walitangaza mapinduzi kwenye televisheni ya taifa muda mfupi baada ya tume ya taifa ya uchaguzi kumtangaza Bongo mshindi.

Forum

XS
SM
MD
LG