Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 10, 2024 Local time: 19:44

Umoja wa Mataifa: Manyanyaso ya kingono Sudan yanatendekea katika kiwango cha kuumiza


Magari ya kivita ya jeshi la Sudan yakiendeshwa barabarani mjini Khartoum, Juni 26, 2023. Picha na AFP
Magari ya kivita ya jeshi la Sudan yakiendeshwa barabarani mjini Khartoum, Juni 26, 2023. Picha na AFP

Manyanyaso ya kingono yanatendwa nchini Sudan kwa kiwango cha kuumiza wakati mapigano katika eneo la Darfur yanafungua tena majeraha ya zamani ya mvutano wa kikabila ambao unaweza kuikumba nchi hiyo maafisa wa Umoja wa Mataifa waliliambia Baraza la Usalama siku ya Jumatano.

Ushuhuda wa kutisha wa unyanyasaji wa kingono ambao umesikika kutoka kwa watu ambao wamekimbilia Port Sudan ni sehemu ndogo tu ya taarifa zinazorudiwa kwa kiwango cha kuudhi kutoka maeneo yenye mizozo kote nchini alisema afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa wa misaada Edem Wosornu.

Vita vilianza Aprili 15 miaka minne baada ya kupinduliwa kwa Rais wa zamani Omar al-Bashir wakati wa uasi wa wananchi. Mivutano kati ya jeshi (SAF) na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) ambao kwa pamoja walifanya mapinduzi mwaka 2021, ulizuka kutokana na kutoelewana kuhusu mpango wa mpito kuelekea utawala wa kiraia.

Forum

XS
SM
MD
LG