Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 05:24

Wasudan wafariki kwa kukosa huduma za afya, mamilioni wakikabiliwa na njaa


Watu wakipanda lori kuutoroka mji wa Khartoum Aprili 28, 2023. Picha na REUTERS.
Watu wakipanda lori kuutoroka mji wa Khartoum Aprili 28, 2023. Picha na REUTERS.

Mamilioni ya watu wanaishiwa na chakula nchini Sudan na baadhi wanafariki kutokana na ukosefu wa huduma za afya baada ya miezi minne ya vita ambavyo vimeuharibu mji mkuu Khartoum na kusababisha mashambulizi ya kikabila huko Darfur, Umoja wa Mataifa ulionya Jumanne.

“Muda unakwenda kwa wakulima kupanda mazao ambayo yatawalisha wao na majirani zao. Vifaa vya matibabu ni adimu. Hali inazidi kudorora," Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamesema katika taarifa ya pamoja.

Mzozo kati ya jeshi la Sudan na jeshi la Vikosi vya Msaada wa Dharura (RSF) uliozuka Aprili 15 kutokana na mivutano inayohusishwa na mpango wa mpito kurejesha utawala wa kiraia, kumeitumbukiza nchi katika ghasia na kutishia kusababisha ukosefu wa uthabiti katika eneo hilo.

Zaidi ya watu milioni nne wamekoseshwa makazi, wakiwemo takribani watu milioni moja ambao wamekimbilia nchi jirani. Raia katika majimbo yaliyoathiriwa na vita wameuawa katika mashambulizi hayo.

"Miili ya watu wengi waliouwawa haijakusanywa, kutambuliwa au kuzikwa,” lakini Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya watu 4,000 wameuawa, msemaji wa Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu, Elizabeth Throssell, alisema katika kikao fupi mjini Geneva.

Ripoti za manyanyaso ya kijinsia zimeongezeka kwa asilimia 50 amesema afisa wa Umoja wa mataifa wa idadi ya watu, Laila Baker.

Mamilioni ya watu waliosalia Khartoum na mijini katika mikoa Darfur na Kordofan wanakabiliwa na uporaji wa hali ya juu na ukosefu wa umeme kwa muda mrefu, mawasiliano na maji kukatika.

Chanzo cha nabari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG