Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 20, 2024 Local time: 04:42

Anga ya Sudan yaendelea yafungwa hadi Agosti 15, kuendelea kuruhusu ndege za dharura kutuwa


Uwanja wa ndege wa Port Sudan, Mei 11, 2023.
Uwanja wa ndege wa Port Sudan, Mei 11, 2023.

Mamlaka ya usafiri wa anga ya Sudan imeongeza muda wa kufungwa anga hadi Agosti 15 isipokuwa kwa ndege zenye misaada ya kibinadamu na zile za  uokozi, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Khartoum umesema katika taarifa yake jumatatu. 

Anga ya Sudan ilifungwa kwa safari za kawaida baada ya mzozo wa kijeshi kuzuka baina ya jeshi la nchi na kikosi cha RSF katikati ya mwezi wa April.

Hata hivyo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Khartoum umekuwa ukitoa nafasi ya kipekee kwa safari za kibinadamu na uokozi kufuatia kibali maalumu kilichopatikana kutoka kwa mamlaka husika.

RSF imewaamuru raia kuondoka katika nyumba zao kwenye mji mkuu upande wa kusini , wakazi kadhaa walisema jumapili wakati mapigano baina ya vikosi vya majenerali wawili wa jeshi vikipambana magharibi mwa mkoa wa Darfur.

Vita baina ya majenerali Abbdel Fattah Al Burhan na msaidizi wake wa zamani kamanda wa RSF jenerali Mohamed Dagalo yameuwa takriban watu 3,900, hiyo ni kwa mujibu wa makadirio na kuwakosesha makazi karibu watu milioni 3.5.

Forum

XS
SM
MD
LG