Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 19:56

Wapiganaji wa kikosi cha RSF wawaamuru raia kuondoka majumbani mwao mjini Khartoum


Wapiganaji wa kikosi cha RSF

Wanamgambo wa Sudan waliwaamuru raia kuondoka majumbani mwao katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, wakazi kadhaa wamesema Jumapili, huku mapigano kati ya majeshi ya majenerali wawili hasimu yakiendelea katika mkoa wa magharibi wa Darfur.

Mkazi wa Khartoum Fawzy Radwan ameiambia AFP “ Wapiganaji wa kikosi cha dharura (RSF) waliniambia nina saa 24 kuondoka eneo hili.”

Amekuwa akiilinda nyumba ya familia yake tangu mapigano yalipoanza mjini Khartoum zaidi ya miezi mitatu iliyopita kati ya kikosi cha RSF na jeshi la serikali.

Vita kati ya mkuu wa jeshi Abdel Fattah-al-Burhan na makamu wake wa zamani, kamanda wa RSF Mohamed Dagalo vimeua takriban watu 3,900, kulingana na makadirio ya awali, na kuwalazimisha wengine milioni 3.5 kuhama makazi yao.

Mapigano zaidi yamekuwa yakifanyika katika vitongoji vya Khartoum vyenye wakazi wengi, na kuwalazimisha wakazi milioni 1.7 kukimbia na kuwalazimisha mamilioni ya wengine waliobaki kujikinga na ufyatuaji wa risasi ndani ya nyumba zao, na huku wakikabiliana na mgao wa maji na umeme.

Mamia ya wakazi waliondolewa kwa nguvu katika nyumba zao katika kitongoji cha kusini mwa Khartoum cha Jabra, wakazi walisema Jumapili.

Jabra na eneo jirani la Sahafa ni ngome ya kikosi cha jeshi cha mizinga ni pia ngome ya RSF inayotumiwa na Dagalo.

Forum

XS
SM
MD
LG