Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 23:29

Sudan: Raia 5 wafariki baada ya mabomu kuangukia nyumba zao


Moshi uliotokana na shambulizi mjini Khartoum, Sudan.
Moshi uliotokana na shambulizi mjini Khartoum, Sudan.

Raia watano waliuawa na mabomu yaliayongukia nyumba zao katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, chanzo kimoja cha matibabu, kililiambia shirika la habari la AFP, siku moja baada ya shambulizi la angani kuua raia wasiopungua 20 kusini mwa mji huo.

Wakazi wa mji huo ulioharibiwa na vita walishuhudia mashambulizi ya makombora Jumapili, wakati vita hivyo, kati ya jeshi na wanamgambo, vikiingia mwezi wake wa tano, kulingana na taarifa kutoka kwa kamati ya upinzani ya kitongoji hicho.

Katika taarifa ya awali, kamati iitwayo neighborhood resistance ilisema waathiriwa hao ni pamoja na watoto wawili, na kuongeza kuwa "miili yao haiwezi kuhamishiwa hospitalini kwa sababu ilikuwa imechomeka vibaya sana, au kuraruliwa vipande vipande katika shambulio la bomu."

Kamati hiyo ilisema kuwa idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka.

Tangu vita vilipoanza kati ya jeshi la kawaida na Vikosi vya RSF mnamo Aprili 15, karibu watu 5,000 wameuawa, kulingana na makadirio ya mashirika yanayokusanya Takwimu za kivita.

Forum

XS
SM
MD
LG