Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 21, 2024 Local time: 05:56

Marekani kutoa msaada wa zaidi ya dola milioni 200 kwa Pembe ya Afrika


FILE - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price March 10, 2022.
FILE - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price March 10, 2022.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price amesema Marekani itatoa msaada wa zaidi ya dola milioni 200 kwa Pembe ya Afrika.

Msaada huo utajikita katika kushughulikia mahitaji ya kibinadamu yanayosababishwa na ukame na mzozo wa kikanda.

Msaada huu wa watu wa Marekani utawawezesha washirika wa masuala ya kibinadamu kukidhi mahitaji katika eneo ikiwemo chakula na lishe, huduma za afya, kufikia maji salama, na ujumla wa usafi wa mazingira.

Katika taarifa yake wizara ya mambo ya nje imesema Marekani bado ina wasiwasi mkubwa kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayoendelea katika eneo hilo.

Ufikiaji wa haraka, kamili, salama na usiozuilika wa wafanyakazi wa kibinadamu ni muhimu ili kutoa msaada kwa wakati unaofaa unaotegemea mahitaji kwa wale walioathiriwa na ukame na migogoro inayoendelea na kuokoa maisha.

XS
SM
MD
LG