Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 06, 2022 Local time: 17:51

Mjumbe wa Marekani katika pembe ya Afrika kujiuzulu


Mjumbe maalum wa Marekani katika pembe ya Afrika David Satterfield

Mjumbe maalum wa Marekani kwa ajili ya pembe ya Afrika David Satterfield, ametangaza kujiuzulu, ikiwa ni miezi sita baada ya kuteuliwa.

Satterfield, anajiuzulu wakati ambapo pembe ya Afrika inakabiliwa na migogoro mikubwa ya kisiasa. Ataondoka ofisini kipindi cha joto.

Naibu wa mjumbe huyo maalum Payton Knopf, atakaimu katika nafasi yake.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema kwamba Satterfield na Knopf wanatarajiwa kuwasili Ethiopia leo Jumatano kwa mkutano na maafisa wa serikali ya Ethiopia, wawakilishi wa mashirika ya misaada na wa kidiplomasia.

Wizara hiyo haijatoa taarifa rasmi kuhusu hatua ya kujiuzulu kwa Satterfield.

Vita vya Ethiopia vimechukua mwaka mzima, na kusababisha shutuma za kila upande kutekeleza mauaji na ukiukaji wa haki za kibinadamu, huku Sudan ikiwa katika mgogoro wa kisiasa na kiuchumi kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Oktoba.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG