Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 14:22

Kituo cha IGAD Somalia chalenga kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa


Rais Mohamed Abdullahi Farmajo
Rais Mohamed Abdullahi Farmajo

Mamlaka ya Maendeleo ya Kieneo - IGAD imefungua kituo cha utafiti nchini Somalia ili kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa. 

Ukame mbaya sana na mafuriko yamewakosesha makazi takriban watu nusu milioni nchini humo Mwaka jana.

Kituo hicho kipya, kipo katika mji mkuu wa Somalia, na kitafanya utafiti, kukusanya data na kutathmini na kusambaza habari mpya kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa katika Pembe ya Afrika.

Rais wa Somalia Mohammed Abdullahi Mohammed, maarufu kama Farmajo, alifungua kituo hicho katika sherehe zilizofanyika Alhamisi. Alisema kitakuwa na mchango mkubwa katika kuisaidia Somalia kukabiliana na changamoto ambazo zinahusiana na mabadiliko ya hali ya hewa.

“Kituo kitalenga katika njia na namna ya kutumia utafiti, data na ufahamu wa kisayansi kulisaidia eneo hilo kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na mazingira. Tumetenga kituo maalum kimkakati na tutakuwa na jukumu kuu la kuhamasisha rasilimali,” amesema Rais Farmajo.

Katika miaka ya karibuni, Somalia imekabiliwa na ukame mbaya sana na njaa, ambayo inahusishwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Workneh Gebeyehu
Workneh Gebeyehu

Katibu Mkuu wa IGAD, Workneh Gebeyehu anasema njaa imeumiza sana harakati za kiuchumi kote katika eneo hilo.

“Hali mbaya sana ya hewa ina athari pana kwa uchumi wa kieneo hasa katika sekta za kilimo na mifugo. Eneo la IGAD ni makazi ya takriban mifugo milioni 520, wanyama wawili kwa kila mmoja wetu, wengi wao wanategemea malisho katika ardhi kavu na mazingira ambayo yamekabiliwa na mabadiliko ya hali ya hewa,” amesema Gebeyehu.

Kuundwa kwa kituo kipya cha IGAD nchini Somalia kunakuja wakati ambapo nchi inakahiliwa na hali ya ukame, mafuriko na baa la nzige, ambayo yote ni mienendo inayohusishwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

XS
SM
MD
LG