Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 05:02

Watu 30 wauawa katika mapigano Somalia


Wapiganaji wa Ahlu-Sunna.

Takriban watu 30 wameuawa nchini Somali huku wengine zaidi ya 1,000 wakijeruhiwa kwenye mapigano yanayoendelea kuongezeka kati ya jeshi la kitaifa na kundi shirika la zamani la Ahlu Sunnah Wal Jama’a(ASWJ), kwenye jimbo la Galmudug mwishoni mwa wiki,

Hayo ni kwa mujibu wa wakazi na maafisa wa kieneo. Harrison Kamau anasimulia zaidi.

Mapigano hayo yametokea kwenye wilaya ya pili kwa ukubwa ya Guriceel wakati kukiwa na hofu ya kuvuruga juhudi zao za kupambana na kundi la kigaidi la Al Shabaab. Mapigano ya karibuni zaidi yametokea mapema Jumamosi na kuendelea hadi Jumapili.

Mmoja wa wakazi kwa jina Farah Abdullahi ameambia shirika la habari la Reuters kwamba amedhibitisha kwamba watu 30 wakekufa kwa kuwa alifahamu 27 miongoni mwao, akiongeza kwamba wametokea kwenye pande zote mbili zinazozozana.

ASWJ ni kundi la waislamu wa Sufi na ambalo limekuwa kwenye mstari wa mbele katika kukabiliana na kundi la al Shabab linalohusishwa na al Qaeda. Hata hivyo hali ya taharuki kati ya kundi hilo na jeshi la serikali imekuwa ikitanda kwa miaka kadhaa sasa wakati likilaumu serikali kwa kutofanya vya kutosha kukabiliana na ugaidi huku serikali ikilaumu ASWJ kwa kufanya mambo bila ruhusa yake.

Hali ilidorora zaidi mapema mwaka huu baada ya vikosi vya serikali kushambulia ASWJ ambalo lilijibu kwa kuteka wilaya ya Guriceel, wakati wakazi wakikaribisha hatua hiyo. Miongoni mwa watu waliokufa mwishoni mwa wiki ni afisa wa ngazi ya juu jeshini Abdi Ladiif Fayfle ambaye ni kamanda wa vikosi maalum vilivyo pewa mafunzo na Marekani.

Maafisa wa afya wamesema kwamba hospitali ya Fayo imepokea majeruhi 30, wakati ile ya Istarlin ikipokea wengine 10. Ile ya Hanano imepokea wagonjwa 60, maafisa wameongeza.

Mfanyakazi mmoja kwenye uwanja wa ndege amesema kwamba ndege ya jeshi ilipeleka wanajeshi waliojeruhiwa kwenye hospitali za mji mkuu wa Mogadishu.

Waziri wa usalama wa jimbo la Galmudug Ahmed Moalim Fiqi mapema mwezi huu alijiuzulu baada ya serikali kupuzia ushauri wake wa kutoshambulia kundi la ASWJ.

XS
SM
MD
LG