Tangazo hilo linakuja baada ya Waziri Mkuu kuongoza kikao cha hali ya juu cha Baraza la Mawaziri Jumanne.
Ametoa wito kwa watu wa Somalia na Jumuiya ya Kimataifa kuwasaidia wale walioathiriwa na ukame.
Ukame mkubwa umepiga katika mikoa kadhaa kwenye nchi hiyo na kusababisha watu na wanyama kuwa katika hali mbaya ya kuhitaji chakula.
Katika baadhi ya maeneo, umesabisha vifo kwa watu pamoja na mifugo.
Umoja wa Mataifa unaripoti kwamba ukame umeongezeka kutokana na ukosefu wa mvua kwa mara ya tatu tangu mwaka 2020.
Takriban Wasomali milioni 3.5 tayari wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa usalama wa chakula, hilo ni kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.