Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 29, 2022 Local time: 03:46

Hali ya ukame yaendelea kudorora Somalia


Familia iliyoathiriwa na ukame Wajaale, Somalia.

Hali ya ukame nchini Somalia inasemekana kudorora licha ya kuwepo kwa mvua katika baadhi ya maeneo kulingana na afisa wa ngazi ya juu kwenye huduma za kibinadamu.

Kulingana na Ian Ridley anayeongoza ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya masuala ya kibinadamu, nchini Somalia, wakati wa mahojiano na VOA amesema mvua za hivi karibuni hazitoshi na kwamba ukame umeendelea kushuhudiwa.

Ridley amekuwa akitembelea maeneo yalioathiriwa zaidi katika wiki za karibuni. Wakati akizungumza kutoka mji mkuu wa Mogadishu, Ridley amesema kwamba visima vilivyoko tayari vimeanza kukauka na kwa hivyo kuongeza hitaji la visima vyenye kina kirefu.

Ameongeza kusema kwamba hali iliyoko imelazimisha watu kuhama makwao, baadhi wakisafiri umbali wa kati ya kilomita 30 na 40 kutoka maeneo ya mashambani hadi kwenye maeneo ya mijini.

Amesema pia kwamba kuna hatari kubwa ya kutokea kwa magonjwa kama vile kipindupindu huku surua ikisemekana kuongezeka miongoni mwa watu walioko kwenye makambi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG