Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 01:53

Somalia yakabiliwa na njaa kali kutokana na uhaba wa mvua, Umoja wa mataifa umesema


Umoja wa mataifa Jumatatu umeonya kwamba karibu mtu mmoja kati ya watu wanne huko Somalia anakabiliwa na njaa kali, wakati ukame unaikumba  nchi hiyo kufuatia uhaba wa mvua.

Hali hiyo inatarajiwa kuwa mbaya sana, na kuwaacha watu milioni 4 na laki 6 wakihitaji msaada wa chakula ifikapo mwezi Mei mwaka 2022, Umoja wa mataifa umesema, ukiongeza kuwa nchi hiyo imekuwa na msimu mbaya wa mvua kwa mara ya tatu mfululizo katika kipindi cha zaidi ya miaka 30.

Uhaba wa chakula, maji na ardhi kwa ajili ya malisho, tayari umewalazimu watu 169,000 kuhama makazi yao, huku idadi hiyo ikikadiriwa kufikia milioni 1 na laki 4 ndani ya miezi 6, Umoja wa mataifa umesema katika taarifa.

Katika miaka ya hivi karibuni, majanga na sio mizozo yamekuwa kichocheo kikuu cha watu kuhama makazi yao nchini Somalia, taifa lililokumbwa na vita ambalo ni miongoni mwa mataifa ya dunia yaliyo hatarini zaidi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

“Ni dhoruba kamili inayokuja, Adam Abdelmoula, mratibu wa misaada ya kibinadamu ya Umoja wa mataifa nchini Somalia”, ameliambia shirika la habari la AFP katika mahojiano, akionya kuwa watu 300, 000 wenye umri wa miaka mitano na chini zaidi wako katika hatari ya utapiamlo mkali katika miezi ijayo.

XS
SM
MD
LG