Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 01:02

Mwakilishi wa Marekani pembe ya Afrika adai vita inazorotesha suluhu ya Ethiopia


Jeffrey D. Feltman, naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani anaehusika na nchi za Pembe mwa Afrika akizungumza mjini Tripoli.

Feltman, aliwaeleza wanahabari kwa ufupi mjini Washington baada ya kurejea kutoka Ethiopia.

Mwakilishi huyo alirejea Jumatatu, ambapo alikutana na waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, na walijadili uwezekano wa suluhisho la kidiplomasia kumaliza mgogoro uliochukuwa mwaka mzima ambao umesababisha vifo vya maelfu ya watu na mamilioni wengine kukimbia makazi yao katika taifa hilo la pili Afrika kwa idadi kubwa ya watu.

Amesema kwamba pande zote yaani serekali ya waziri mkuu Ahmed, na TPLF wanaona njia pekee ya kupata ushindi ni mapigano ya kijeshi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG