Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:10

Jinsi zao la teff lenye asili yake Pembe ya Afrika lilivyopata umashuhuri Marekani


Mkulima Tesfa Drar akiwa karibu na mashine ya kumwagilia katika shamba linalootesha teff kaskazini mashariki ya Nevada. Kampuni yake, Selam Foods, inauza nafaka ya kale ya asili katika nchi za Pembe ya Afrika , Oct. 2021.
Mkulima Tesfa Drar akiwa karibu na mashine ya kumwagilia katika shamba linalootesha teff kaskazini mashariki ya Nevada. Kampuni yake, Selam Foods, inauza nafaka ya kale ya asili katika nchi za Pembe ya Afrika , Oct. 2021.

Teff, nafaka ya kale ambayo asili yake ni Pembe ya Afrika, imepata washabiki wapya nchini Marekani. Inalimwa Magharibi na Magharibi Kati mwa Marekani, ambako wakulima wanaeleza inaendelea kuvutia kama chakula kisichokuwa na gluten “chakula bora.”

Mmoja wa wakulima hao ni Tesfa Drar, ambaye alikuwan akiwasaidia wazazi wake kupanda teff sehemu ambayo hivi leo inajulikana kama Eritrea

Alipokuja Marekani kusoma mwaka 1981, alikuwa ana hamu ya injera, mkate unaotengenezwa na unga wa teff ambao ni chakula kikuu cha Pembe ya Afrika.

“Hivyo, niliamua kuja na paundi 20 [za teff] kutoka nyumbani na kupanda katika eneo la Chuo Kikuu cha Minnesota, ambako nilikuwa nasoma,” Tesfa anakumbuka, akiwa amesimama katika shamba la nafaka lililioko katika jimbo la kaskazini la Nevada. “Kuanzia wakati huo, nilitoa mbegu kwa vyuo vikuu mbalimbali kwa ajili ya utafiti.”

Alipofika Marekani kuanza chuo mwaka 1981, alikuwa hawezi kupata injera, mkate laini, wa unga wa teff ambao ni chakula kikuu cha Pembe ya Afrika.

Hivi sasa masoko yake ya Selam Foods nafaka iliyo na virutubisho vya chuma inapatikana kupitia kwenye mtandao, na inayo tovuti inayoonyesha aina mbalimbali za mapishi ya injera na historia ya teff, moja ya mimea ya kale inayotumika kwa chakula cha nyumbani.

Mkate wa injera uliyotengenezwa kwa teff, Oct 2021.
Mkate wa injera uliyotengenezwa kwa teff, Oct 2021.

Tesfa anapanda nafaka hiyo katika eneo lenye ekari zaidi ya 2,400 hapa Nevada, na Minnesota – ambako kampuni ya Selam Foods ina makao yake makuu – na katika majimbo mengine sita. Operesheni zake hapa kaskazini magharibi mwa Nevada ni karibu na Winnemucca, mji wenye biashara ya kamari kwa saa 24 na pia jumuiya ya wakulima ambao wanajishughulisha na kulima viazi ulaya, alfalfa, ngano na mahindi.

Lakini hivi sasa wakulima wengi zaidi wameingia kutumia fursa ya mahitaji katika soko la chakula kisichokuwa na gluten kwa kupanda teff. Ekari zinazolimwa teff “zimeongezeka” katika miaka ya karibuni, kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Nevada – Reno, inayoeleza kuwa nafaka hii hivi sasa inalimwa takriban katika majimbo 25 ya Marekani.

Katika barabara kutoka eneo la Tesfa, kwenye jangwa la Oasisi Teff na Grain in Fallon, John Getto na mtoto wake wa kiume Myles wanasema wao wanalima “nafaka za kale kwa ladha ya kisasa.” Wanauza teff kwa malori kwa wanunuzi wa jumla huko California na mfuko wa paundi moja kwa walaji wa eneo hilo au kwa njia ya mtandao.

“Nevada ina hali ya hewa nzuri kwa kilimo cha teff, ambayo ni sehemu nzuri,” Myles Getto alisema. “Ni sehemu yenye joto. Joto sana. Mvua ni chache, lakini tunamwagilia mashamba yetu ya teff. Ni hali ya hewa nzuri kwa kilimo cha teff.

John Getto na mtoto wake Myles Getto wakiwa katika eneo la biashara Fallon, Nevada, Oct. 2021.
John Getto na mtoto wake Myles Getto wakiwa katika eneo la biashara Fallon, Nevada, Oct. 2021.

Watafiti wa Chuo Kikuu cha Nevada-Reno wanashughulikia kuanzisha aina mbalimbali za teff inayohimili ukame na kukua kwa muda mfupi. John Cushman, profesa ambaye anasimamia programu ya shahada ya biochemistry, alisema hilo lilikuwa ni muhimu kwa wakulima wanaoishi katika jimbo kavu Marekani.

“Tuligunda kuwa kulikuwa na mahitaji makubwa ya aina ya mazao ambayo yanatumia maji kiasi,” alisema, “ambapo upande wa magharibi mwa Marekani unakabiliwa na ukame zaidi na ukame huo unasababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, tulihisi ni muhimu kuwekeza katika baadhi ya mazao mbadala.

Bob Dexter ameongeza zao la teff katika ardhi anayolima pembezoni mwa Mto Carson.

“Nilikuwa nataka kupanda kitu kingine mbali na chakula cha ng’ombe,” Dexter alisema, ambaye kwa kawaida alikuwa analima ngano, shayiri na alfalfa. “… Nilikuwa nataka kulima kitu kizuri kwa ajili ya watu kula. Nilipogundua kuhusu teff, ilionekana ni muafaka kwa kile tulichokuwa nacho hapa kuendana na hali ya hewa yetu.”

Teff, majani yake yakiwa na mbegu, Oct. 2021.
Teff, majani yake yakiwa na mbegu, Oct. 2021.

Dexter amesema mara mbegu zake zinapovunwa, baadhi ya mavuno ya teff(teff hay) ni chakula kinachohitajika kwa wanamiliki farasi ambao wanataka kupunguza sukari katika vyakula vya wanyama wao.

“Farasi wanapenda teff hay. Kwa ujumla ina harufu nzuri, “ alisema, akiongeza kuwa ni zao bora zaidi kuliko alfalfa “kwa sababu lina kiwango cha chini ya kabohydrate ambacho kinasababisha farasi kupata matatizo ya kiafya.

Kiwango kikubwa cha teff inayozalishwa nchini Marekani inakwenda kwenye lishe, kulingana na Chuo Kikuu cha Nevada- Reno. Nafaka inavyoweza kutumika inaongeza thamani kwa wakulima wa Nevada, Cushman alisema: Teff siyo tu inatoa kiwango cha juu cha lishe kwa uzalishaji wa mifugo, lakini pia inatupa lishe yenye virutubisho vya juu kabisa, yenye utajiri wa madini ya chuma na nafaka isiyokuwa na gluten ikiwa ni faida ya ziada kwa lishe ya mwanadamu.

Kampuni ya CSS Farms imeongeza teff katika mzunguko wake wa uzalishaji viazi, alfalfa na ngano. Meneja mkuu Kyle Noise alisema kuwa kampuni hiyo itapanda nafaka hiyo zaidi msimu ujao, ikitambua umaarufu wa nafaka hiyo kwa wahamiaji kutoka nchi nyingi zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara, idadi inayoongezeka kwa kasi ya watu hao nchini Marekani.

Teff kutoka mashariki ya Afrika
Teff kutoka mashariki ya Afrika

“Naona kuna mahitaji mazuri kwa zao hili kusonga mbele, hususan kwa kuwa halina gluten,” alisema. “Kuna matumizi mengi ya zao hili.”

Ukuliangalia soko kwa zao la teff linapanuka kuanzia kwa diaspora ya waa Afrika Mashariki hadi kwa walaji wenye umakini wa afya zao, Tesfa Drar alisema kadiri kiwango cha fiber kinavyokuwa juu “chakula bora” kina hitajika duniani.

Teff inaweza kutumika kwa kutengeneza biskuti, kwa kutengeneza keki, uji na unaweza kutengeneza pizza,” Tesfa alisema. “… Sasa tunafanya kazi na Pizza Hut ili kuwauzia teff isiyokuwa na gluten ili itumike kutengeneza pizza.

Trésor M. Matondo amechangia katika repoti hii.

XS
SM
MD
LG