Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 25, 2024 Local time: 12:23

Mahakama ya kijeshi Tunisia yahukumu mbunge kwenda jela kwa kumtusi rais


FILE - Rais wa Tunisia Kais Saied akihutubia katika ziara yake huko mjini Sidi Bouzid, Tunisia, Sept. 20, 2021.
FILE - Rais wa Tunisia Kais Saied akihutubia katika ziara yake huko mjini Sidi Bouzid, Tunisia, Sept. 20, 2021.

Mbunge wa bunge lililosimamishwa shughuli zake Tunisia, Yassin Ayari, ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa mahakama ya kijeshi Jumamosi imemhukumu bila ya kuwepo mahakamani kutumikia kifungo cha miaka 1o jela kwa mashtaka ya kumtusi rais na jeshi baada ya kueleza hatua ya rais kusimamisha shughuli za bunge ni kitendo cha mapinduzi ya kijeshi.

Rais Kais Saied alisimamisha shughuli za Bunge hilo Julai 25, aliivunja serikali na kuchukua udhibiti wa mamlaka yote, na kupelekea kukoselwa ndani ya nchi na nje.

Adhabu ya kifungo iliyotolewa inaongeza hofu ya upinzani kuwa Saied anataka kulipiza kisasi kwa wapinzani wake, baada ya kulivunja Baraza La Juu la Mahakama – chombo kinachotoa dhamana ya uhuru wa mhimili wa mahakama. Ayari katika ujumbe aliouweka kwenye mtandao wa Facebook alielezea vitendo vya Saied kama mapinduzi ya kijeshi.

“Ni kejeli. … Jana Saied alisema huko Brussels kuwa yeye siyo dikteta na leo mahakama ya kijeshi inatoa adhabu ya kifungo dhidi ya uhuru wa kujielezea kwa mbunge,” Ayari ameiambia Reuters kwa simu kutoka Paris.

Wakosoaji wa Saied wanamtuhumu kwa kutaka kutawala kidikteta na kukandamiza utawala wa sheria.

Saied alisema ataendeleza haki na uhuru aliposhinda katika mapinduzi ya 2011 yaliyoleta demokrasia Tunisia na ataweka katiba mpya kupitia kura ya maoni wakati wa majira ya joto, huku uchaguzi wa bunge ukifuatia mwezi Disemba.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG