Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Agosti 17, 2022 Local time: 11:39

Kibali cha kukamatwa chatolewa dhidi ya aliyekuwa rais wa Tunisia


Rais wa Tunisia Kais Saied.

Serikali ya Tunisia imetoa kibali cha kukamatwa dhidi ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Moncef Marzouki.

Kibali hicho kimetolewa mwezi mmoja baada ya kutoa wito kwa Ufaransa kusitisha msaada kwa serikali aliyovunjilia mbali mwezi July.

Rais Kais Saied aliamurisha wizara ya haki kuanzisha uchunguzi dhidi ya Mazouki mwenye umri wa miaka 76, siku chache baada ya kiongozi huyo wa zamani kutaka Ufaransa kutosaidia utawala wa kiimla war ais Saied.

Televisheni ya taifa ya Tunisia haikutoa sababu za kutolewa kwa kibali hicho cha kukamatwa na waendesha mashtaka hawajatoa taarifa yoyote.

Marzouki, ambaye aliishi nchini Ufaransa kwa mda wa miaka 10 wakati wa utawala wa Zine El Abidine Ben Ali, amesema kwamba hababaishwi na hatua yoyote inayochukuliwa na utawala wa Tunisia.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG